Jumamosi, 18 Mei 2013

NDOA ZA JINSIA MOJA RUKSA UFARANSA, WA KWANZA KUONANA NDANI YA SIKU 10

Mashoga wana haki ya kuwatunza watoto, hali kadhalika kwa wasagaji ambapo wanaweza kuoana. Hatua hiyo ni baada ya Rais François Hollande kuweka saini ya kupitisha muswada huo kuwa sheria, ambapo licha ya mvutano wa  baadhi ya asasi na mashirika yasiyo ya kiserikali, Rais Hollande ametimiza ilani ya uchaguzi ya chama chake, ambapo aliahidi kufanya hivi endapo atachaguliwa.


wasagaji wakiwa wameoana
Siku kumi zijao, zinatarajiwa kutokea kwa watu watakaofunga ndoa ya namna hiyo, ikiwa ni katika kuweka rekodi nchini humo, kwa kuwa sheria hiyo itaana kutumika baada ya siku hizo.

mojawapo ya maadamano ya kushinikiza ndoa za jinsia moja nchini Ufaransa mwaka jana. © Lionel Bonaventure,
Pamoja na changamoto ambazo chama pinzani cha  rais wa zamani wa nchi hiyo ha UMP, Nicolas Sarkozy, bado Rais Hollande hakuona kizuizi kuweka saini hiyo, ambayo inaifanya Ufaransa kuwa nchi ya 14 kuidhinisha ndoa za namna hiyo.
Ramani ikionesha nchi zinazoruhusu ndoa za jinsia moja, rangi ambazo hazijakolea zikitofautiana kulingana na maeneo.
Tayari kunatarajiwa kuwa na maandamano makubwa tarehe 26 mwezi Mei, siku mbili kabla ya kushudiwa kwa ndoa za namna hiyo zikifugwa kwa mara ya kwanza nchini humo, ambapo inatarajiwa kuwa maandamano hayo yatakuwa makubwa kuliko ilivyowahi kutokea.

mojawapo ya maandamano yaliyowahi kufanyika jijini Paris, kupinga ndoa za jinsia moja. msisitizo  'un papa + un maman,.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo, ni ngumu kwa sheria hiyo kuondolewa hata kama uongozi mwingine utashika dola kutokana na madhara ambayo yatajitokeza, na hivyo hata maandamano hayo yanaonekana kwamba yatakuwa na athari chache.

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595