Picha hii ndiyo ya sura ya kanisa kwasasa wakati ujenzi ukiendelea
Kwa hakika hizi ni habari njema, kwamba kumbe watanzania wanaweza
kufanya mambo makubwa ya maendeleo pasipo kutegemea misaada kutoka nje ya nchi,
ukweli huu unathibitika waziwazi kwa waumini na washirika wa kanisa la Tanzania
Assemblies Of God tawi la Tabata lililoko jijini Dar es salaam,
Jumapili hii, kulifanya harambee ya ujenzi wa kanisa TAG
tawi la Tabata, Mchungaji kiongozi Rony Swai wa kanisa ilo alianza ibada hiyo
ya changizo kwaajili ya ujenzi kwa kusoma Neno la Mungu kutoka katika kitabu
cha 1Nyakati 22:1-5, akifanunua maneno hayo ya Mungu, alisema Tunamjengea Mungu
wetu nyumba nzuri na yenye utukufu wake hapa Tabata, na kwakuwa tunamheshimu
ndio maana tunajenga kanisa zuri ambalo litakuwa na kila huduma muhimu wakati
wa ibada kama vile (AC) kiyoyozi, kwa ramani na mwonekano katika picha kanisa
letu litakuwa na uwezo wa kuketisha watu elfu moja kwa wakati mmoja, hapa
jijini na Tanzania, yapo makanisa yenye uwezo wa kuketisha watu wengi kuliko
idadi hii niliyoitaja, lakini tofauti yetu na hayo makanisa ni ule ubora na
uzuri wa jingo, kanisa letu litakuwa zuri kuliko makanisa mengine yote hapa
Tanzania, kwasababu tumependa kumheshimu Mungu kwa njia hii pia. Kanisa la
mahali hapa, litaleta matumaini katika Taifa la Tanzania na nje ya nchi
Ni vema wananchi wote wa Tanzania katika maeneo yetu au
makazi yetu, tujaribu kuiga umoja na kama wanao uonyesha ndugu zetu wa TAG
Tabata, kama kuna tatizo la ubovu wa miundo mbinu ya barabara mtaani kwetu,
tushilikiane kukarabati barabara hiyo, kama kuna tatizo la uchakavu wa majengo
ya shule katika maeneo yetu iwe ni vyoo au madarasa, na kukarabati, wakati
mwingine tunaposema Serikali itafanya ni kama kujichelewesha wenyewe katika
maendeleo yetu, hakuna asiye elewa kuwa bado pato letu kama Taifa bado ni dogo,
kwahiyo pale tunapo weza kutumia rasilimali ya umoja ni nguvu, ni bora kufanya
hivyo. Kwa hakika kumbe inawezekana kufanikisha hata ujenzi wa zahanati katika
kijiji chetu pasipo nguvu ya fedha kutoka serikalini, kwani hawa TAG tabata wao
wamepata msaada serikalini, jibu ni la, ni umoja wao na moyo wao wa uzalendo
kwaajili ya kanisa lao
Sauti ya kanisa inachukua nafasi hii kumwomba mtu yeyote
kuwaombea ndugu zetu hao wa Tabata TAG, ili wafanikishe ujenzi wa kanisa lao,
lakini pia ni vema kwa yeyote anayependa, tuwatie moyo kwa kuwasaidia katika
kile wanacho kifanya, kama utapenda, basi fika kanisani hapo siku yoyote na
utawakuta wahusika wakiendelea na ujenzi. namba ya simu ya kanisa ni 0784520968
Hii ndivyo itakavyo kuwa mara baada ya ujenzi wa kanisa la TAG Tabata, kwahakika inapendeza sana, na inaonyesha kwamba watanzania twaweza, mimi nikutakie siku njema na kila la heri kwa yote mema uyafanyayo kwa kusema, MOYO WA KUJITOLEA NA UZALENDO ULETA MAENDELEO KWAKO NA KWA WENGINE