Jumapili, 1 Septemba 2013

HABARI PICHA ZA JINSI ASKOFU KULOLA ALIVYOAGWA DAR ES SALAAM



sehemu ya waombelezaji, na waliovaa nguo nyeusi ni wajukuu wa Askofu Kulola waliwa katika huzuni ya kuondokewa na babu yao waliyempenda

Makamu wa Rais akitoa rambirambi kwa niaba ya serikali kwenye msiba wa Askofu kulola, amesema amemfahamu kulola kwa miaka mingi, lakini kubwa ni kwamba kulola ameisaidia sana Tanzania kuleta amani kutokana na mahubiri yake alisema makamu wa Rais

watu walikuwa wengi sana katika msiba huu, hapa wengine wanalia na wengine wanaimba nyimbo za maombolezo

msiba huu umefanya hata wale walikuwa hawakutani kukutana, kutoka kushoto ni mchungaji Gwajima, kakobe, lusekelo na ndegi wakiwa katika msiba wa Askofu Kulola, wamepiga picha wakiwa wamekumbatiana

umati wa waombolezaji wakiwa ndani ya hema mojawapo katika viwanja vya kanisa la Eagt Temete

jengo linalo onekana ndilo kanisa la Eagt Temeke, mahali ambapo Askofu kulola alipokuwa anaabudu mara nyingi akiwa Dar es salaam, tungesema ndilo kanisa mama lililozaa kanisa la Eagt Tanzania na nje ya Tanzania
Philip Mangula akitoa salamu za rambirambi, pia aliwaongoza waombolezaji kuimba pambio, alivuta hisia za watu wengi kutokana ujuzi wake wa kuimba pambio

katibu mkuu wa Chadema akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo na kuandika mambo machache ya kumbukumbu kuhusu kulola

katibu mkuu wa PCT Askofu Mwasota na Askofu Mitachi wakiteta jambo kuhusiana na kuondokewa na kipenzi chao

watumishi wa Mungu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuaga mwili wa Askofu Kulola jijini Dar esa salaam
Askofu Gamanywa akimfariji mke wa Askofu Kulola

ndani ya jeneza linaloonekana, ndimo ulimolazwa mwili wa Askofu Moses Kulola

katikati ya hao akina mama, kushoto mwa jeneza aliyevaa mavazi meupe, ndiye mke wa Askofu Kulola, aanashuhudia jeneza la mume wake mbele ya macho

huu ndio mwili wa Kulola, ni kama amepumzika tu ataamka tena na kuendelea kuhubiri na kusema hiyooooooo, ukitazama alivyo vaa utafikiri yupo hai, amevaa mavazi kama yale aliyokuwa anavaa kwenye ibada
m

wengine hawakuvumilia kumtazama Askofu Kulola katika umauti ulimkuta, kwahiyo watu wengi walikuwa wanazima

Ndegi, hivi kweli baba yetu amefariki!! ndicho anachosema mzee wa upako Lusekelo kwa nabii Ndegi

Mh. Mbunge, Dr Getrude Rwakatare.
1976, alipohubiri nilikuwa na matatizo ya ndoa, nilipookoka bado nilikuwa na mateso ya ndoa, nikamuuliza mbona hivi? Akachukua jukumu la kuniandikia barua moja kila mwezi, na kuniambia hakupigi wewe anampiga Yesu, hakutesi wewe, anamtesa Yesu. Alinitia moyo hadi nilipokuwa mchungaji.

Alipokuwa anapelekwa India kwa ajili ya matatizo, nilipata nafasi ya kwenda kumuona Chanika, akaniombea na kunitamkia maneno kwa dakika 15, nikaona kama nimependelewa, na maneno ya mwisho na usia ili niweza kuendelea kumtendea kazi Mungu.

Baba amefanya kazi nzuri sasa ni sisi kuweza kufanya kazi ya BWANA bila kujihurumia.
Bishop Dr Methud Lyamungu, Methodist Church
NImekuwa nikimfahamu Kulola, juzi tu nilipofika uwanja wa ndege nikapokea msg kuwa hatunaye, amepumzishwa, ilikuwa shock, lakini namshukuru Mungu.
Nakumbuka miaka ya late 80's kulikuwa na mkutano kwenye kanisa la udugu, nikamwalika kwa chakula cha jioni, alikuja, nikashangazwa na unyenyekevu wake, ni rafiki wa wote, hana adui.
Askofu Esambu Mitachi Polo;
Bila Kulola sijui ningekuwa wapi, huduma yangu imeinuliwa na makanisa ya Ask. Moses Kulola. Lakini mkumbukkue hivi ndugu zangu, msafara wa mamba, kenge wapo. Yesu ndie muweza yote na yeye ndiye aliyezungumza haya.

Tunaweza kuzungumza maneno mazuri, lakini matendo hatuna. Tumtazame Yesu, maana hata huyu aliyetuacha, alikuwa anatuasa tumtazame Yesu, huwezi kuingia mbinguni bila mamlaka ya Bwana Yesu, usiwe kenge.

Tanzania tumtazame Yesu. Moses amekwenda, lakini Yesu yupo, amefanya kazi zake atalipwa na Bwana Yesu, na wewe ufanye kazi zako utalipwa na Bwana Yesu. Kiburi kitu kibaya, unafiki kitu kibaya, haya ndio maneno nayosema kwa Watz.
Phillip Mangula (makamu m/kiti wa CCM bara)
Moses nimeanza kumfahamu 8/8/1983 nikiwa mkuu wa wilaya ya Kwimba, kipindi kile mtakumbuka kulikuwa n tofauti kidogo ndani ya kanisa, barua iliandikwa nchi nzima ya kuzuia Moses Kulola asihubiri kwa jina la kanisa, na mi niliipata kwangu.
Nikamweleza Moses Kulola, akaniambia, kijana wangu, mimi sitahubiri kwa jina la kanisa lolote, nitahubiri kwa jina la Yesu.

Nikawaita OCD, kwamba bwana, Moses Kulola hatahubiri kwa dhehebu lolote, atahubiri kwa jina la Yesu.

Tareje 9, tumemaliza mkutano, alihubiri mkutano mkubwa sana, mke wangu akajifungua mtoto wa kiume, nikamwita Moses, kwahiyo mtoto wangu anaitwa Moses Malumbo Kulola.
Dakika 20 baada ya kifo cha Dr Moses Kulola, nilipata msg, wakati huo nilikuwa nimetoka Njombe kumzika binti yangu wa mwisho, kipindi ambacho Moses, mtoto wangu alikuwa anaoa, Moses anao, dada yake mdogo anafariki, kwahiyo nilichelewa kidogo, lakini nimefika kushuhudia.

Alipotoka India alikuja na mwanae huyu hapa, tulizungumza mengi sana, lakini haoa si mahala pake, itoshe tu kusema, Moses alikuwa mtu wa watu. Aliendeleza injili, nasi tuiendeleze.
Theresia Uvinza
Nimemfahamu 1985, baada ya kumaliza chuo kikuu nilienda kufundisha Songea Girls, na hapo kulikuwa na rafiki yangu, Mama Hyela, walokole wa kwanza Songea. Siku moja aliomba nimshikie wanafunzi kwa kuwa mchungaji alikuwa anafikia kwake.

Nikamuuliza huyu mchungaji anafanana na Yesu?Akasema pengine, ila ukitaka kumuona, unaweza maana amefikia kwangu. Tukawaacha wanafunzi wote, tulifanya hilo kosa…

Tukasubiri na kusubiri na mida ya saa tisa, alipotoka nikajisikia kupiga magoti, nikamwambia baba naomba uniombee – na kweli akaniombea, nilikuwa na shilingi elfu moja tu, nikampa. Naamini mafanikio niliyo nayo ni kutokana na maombi niliyofanyiwa mwaka 1985.

Kwa hiyo kila wakati ambapo nilikuwa nikisikia Moses Kulola amekuja DSM, kwenye viwanja vya Jangwani , huwa sikusita kuhudhuria, labda tu niwe nje ya Dar. Nakumbuka aliwahi kusema nywele zake zilikuwa zinampotezea muda, hivyo akamuomba Mungu zibaki hivyo hivyo, na kweli zikabaki. Huu ni ushahidi kwamba kuna alikuwa anazungumza na Mungu.
Advera Senso (Msemaji wa Jeshi la Polisi)
Hata kama leo tungeamua takamate watenda dhambi wote, si kwamba wangebadilisha matendo yao kiroho na kimwili.

Amekuwa pia akimbwambia IGP Said Mwema, kuwa unpoona makosa ya jinai yanaongezeka hizo sisi watumishi wa Mungu tunaita dhambi, amwambie ili atume watu ama aende mwenyewe kuhubiri.


Hivyo tumekuwa tukiona makosa yakizidi sehemu, tunawasiliana na yeye anaenda kuhubiri injili eneo hilo.

IGP anasema chipukizi waendelee kuhubiri injili, hadi kweny ngazi ya familia, kwasababu wahalifu wako kwenye familia, wako kwenye mitaa…


Na watu wa Mungu niwawambie kuwa tushirikiane na serikali kuhakikisha kuwa wahuni wachache hawabadilishi amani iliyopo. Tuendelee kuhubiri na watu waokoke.

Paulo
Nashangaa kwa nini nimekuuja hapa, nitazungumza kidogo tofauti na m/kiti wangu.
Nilianza kumfahamu kaka yangu mwaka 67, akiwa ndio ameanza kazi kipindi hicho, nikawa namshangaa sana, nasema huyu mbona anapoteza muda, anazunguka na baiskeli huku na huko nikasema hapa tuna kazi kilichonipa faraja ni pale nilipoanza kuanza kazi yake.

Faraja niyoipata ni pale alipokuja Kilimanjaro, kipindi ambacho alinyimwa kuhubiri. Akaja kunionmba msaada ofisini, nikamwambia nani amekwambia akasema, aah aah, ni hilo ni nimekufikishia.

Nikamwambia kwa jina la Yesu utahubiri. Tukasimamia akafnya mkutano mkubwa sana, na lipomalia akaja ofisini kwanguna kuniambia sina cha kukulipa, piga magoti.

Akaniambia nitakuwakiongozi mzuri, baada ya hapo haikuchukua muda nikapelkwa Mbeya kama mkuu wa mkoa. Baraka zikaendelea, nikapata na uwairi, na tena uwaziri mwingine… nikakoswakoswa kidogo niwe waziri mkuu.
Assumpta Mshama (Mh Mbunge Nkenge/Mchungaji Msaidizi, Mito ya Baraka)
Watz, hatuna haja ya kuendelea kulia, sanasana ni kumshukuru Mungu… Hata ubunge huu nilipoupata, ni kipande kidogo cha Mzee huyu…

Wakati naokoka, 1989 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, nilipoongozwa na mtu ambaye hata pia hajaokoa.

Nilipookoka kazi yangu ilikuwa ni kupika chakula na kumpelekea mahali popote. Na pia baadae nikaanza kurekodi video za mikutano yake.

Nilipotaka kuwa Mbunge, akaniambia utakuwa mbunge – na nilifanikiwa.
Mary Alice Chipungahelo (former RC, DSM)
Nilipoteuliwa kuwa RC, wakaniambia utaweza, nikasema zaidi ya hilo, nitapambana usiku na mchana…

Baba, sasa ni hayati Moses Kulola, alikuwa karibu na mimi sana, na kila anapokuja DSM, lazima anitembelee, Baba huyu, nilikuwa na matatizo, “mwanamke naye nini, mwanamke naye nini”
.
Alikuja nyumbani, nikamkaribisha nikapiga magoti, akauliza una nini, nikamwambia nataka natakasika. Mungu alizidi kuniunganisha naye, nikiwa Mwanza, aliwekwa ndani, nilipopata taarifa, tukapelekeana simu – lakini kama unavyojua kila mka na taratibu zake. Tulikubaliana mzee akatolewa, na akaja kunitafuta ili anie shukurani, nikamwambia hapana shukurani mpe Mungu, maana ndio ametuwezesha.

“Piga magoti” akaniambia, “unataka nini”, nikamwambia nataka niwe na afya nifanye kazi bila upendeleo wala rushwa.

Na ikawa hiyvo, nikapaishwa hadi Canada nikawa msaidizi wa Balozi, kazi ya heshima sana. Nimekuja kw moyo mweupe kabisa moyo mkunjufu, mama nikwambie kuwa wajane tuko wengi, wewe umebahatika kuwa na mzee anayeikjua dini, sisi wengine tumeolewa olewa tu…
Tunakutakia kila kheri, afya njema, ulee watoto, na watoto nao wana watoto wao…





2 comments:

  1. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma

    Kwaheri Gerd Ulrich

    JibuFuta
  2. Habari zenu. Ilikuwa ngumu sana kwangu wakati mpenzi wangu aliniacha kwa mwanamke mwingine. Niliharibiwa kihisia, nilivunjika moyo na sikujua la kufanya ili kumrudisha. Nilihangaika kwa miezi mingi na niliendelea kutafuta msaada kutoka kila mahali hadi nilipopata kujua kuhusu DR DAWN. Niliwasiliana naye na kumweleza shida zangu. Alikuwa tayari kunisaidia na kunisisitiza nifuate taratibu ili aweze kurejesha penzi kati yangu na mtu wangu na pia kuhakikisha tunarudiana wote wawili. Nilipata mahitaji yote na ilifanya kazi hiyo. Baada ya saa 48, nilipata ujumbe kutoka kwa mpenzi wangu akiniuliza tarehe. Sasa tuko pamoja tena na shukrani zote kwa DR DAWN. Anaweza kukusaidia kumrudisha mpenzi wako,
    Anaweza kukusaidia na uchawi wa ujauzito,

    Anaweza kukusaidia kuponya aina yoyote ya ugonjwa.

    ikiwa uko tayari kuamini na kubaki na matumaini. Watumie barua pepe tu kupitia: dawnacuna314@gmail.com
    WhatsApp: +2349046229159

    JibuFuta

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595