Nimeshuhudia na pengine nawewe umeshuhudia, hata mheshimiwa
J.J. Mnyika naye pia ameshuhudia shughuli inayofanyika chini na pembezoni mwa
nyaya zenye umeme mkubwa pale ubungo, na sio tu mheshimiwa mbuge wa Ubungo,
hata mheshimiwa waziri mwenye dhamana ya usalama wa raia na mali zao naye pia
ameona biashara inayofanyika hapa na umati mkubwa uliopageuza mahali hapa pa
hatari kuwa sehemu ya soko kubwa lenye wateja wengi, viongozi wetu kwanini
tunahatarisha maisha ya watu kiasi hiki, wametuchagua kwa lengo moja kubwa,
kwamba muweze kuwatumikia na kuwaongoza kipi cha kufanya na kipi cha
kutokufanya, au kinacho subiriwa hapo ni nini, labda ni kusema maafa makubwa
yatokea Ubungo, tunaomba viongozi wa dini wamwombe ili wale wote waliopatwa na
majanga wapone haraka, je hiyo ni sawa?
Kuna kipindi cha hivi karibuni serikali kwa kutumia jeshi la
polisi, ilipiga marufuku mtu kufanya biashara maeneo hayo, na kulitokea
pulukushani za hapa na pale, lakini kwa vile mkono wa serikali ni mkubwa, wote
waliokuwa wanafanya biashara maeneo hayo walitii na kutoweka maeneo haya,
lakushangaza wale waliambiwa waondoke na sasa wamekuja wengine, sijui ni
walewale au wengine.
Tunaomba wahusika wachukue hatua za haraka na wale wote
wanajihusisha na biashara maeneo haya tukumbuke kwamba uhai ni jambo la thamani
kuliko biashara tunayoifanya.
Mchungaji mmoja alikuwa anahubiri hadi machozi yanamtoka,
akiwambia watu juu ya madhara yatakayo wapata watenda dhambi, akiwaonyosha
mifano mingi ya sodoma na gomola, wale waliosikia waliokolewa lakini waliosema
hakuna kitu tufanye dhambi, waliangamia, si unakumbuka hata habari za Nuhu na
ile safina?
0 comments:
Chapisha Maoni