MTUME VERNON FERNANDES,JOHN LISU NDANI YA ARUSHA
Mtume Fernandes mkono wa kuume akifundisha hapo jana. |
Katika ufunguzi wa kongamano hilo linalohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wafundishaji kutoka ndani na nje ya nchi, Mtume Fernandes alifundisha kuhusiana na umiliki, ukiwa kama mtoto wa Mungu na kumkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako wewe ni mmiliki wa Ufalme wa mbinguni. Wafundishaji wengine watakaosimama katika kongamano hilo ni pamoja na Mchungaji Paul na mkewe Martha Sulley, Mchungaji John Mathenge, Mchungaji Price Mobutu pamoja na waimbaji wengine kama Tumaini Shangilieni kwaya ambao walihudhuria hapo jana, kutoka jijini Dar es salaam The great John Lisu atahudhuria pia, Kingdom kwaya na waimbaji wengine.
Kongamano hilo hufanyika baraka kwa watu wanaohudhuria tangu kuanza kwake miaka ya karibuni, ambapo kwa mara nyingine waandaaji wanamwamini Mungu kwamba atakwenda kufanya kitu katika maisha ya watu wote watakaohudhuria kongamano hilo linalotarajiwa kuhitimika siku ya jumapili tarehe 21/04/2013.
0 comments:
Chapisha Maoni