MAMA aliyempiga mwanaye wa miaka saba hadi kifo kwa kushindwa ‘kukariri kwa kichwa’ mistari ya Quran Tukufu amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Ilielezwa mahakamani kwamba baada ya kubaini kuwa
kipigo hicho kimesababisha kifo cha mwanaye, mama huyo, Sara Ege (33)
alichukua uamuzi wa kuuchoma mwili wake ili kuficha ushahidi.
Baada ya kusomewa hukumu hiyo, mama huyo alizimia
kizimbani hivyo kulazimika kusaidiwa kwa kuondolewa katika kizimba cha
mahakama hiyo, baada ya kuelezwa kwamba hatahusishwa kwenye msamaha wa
aina yoyote hadi atakapotumika miaka 17 gerezani.
Mahakama hiyo ilielezwa kwamba mama huyo
alimnyanyasa mwanaye “kama mbwa” wakati alipokuwa akihangaika angalau
kukumbuka kwa kichwa mistari michache ya kitabu hicho kitukufu cha dini
ya Kiislamu.
Ilielezwa kwamba aliendelea kumuadhibu kwa kumpiga
kwa miezi mitatu mfululizo akimlazimisha kukariri mistari ya kitabu
hicho, hadi alipodondoka akiwa chumbani kwake huku akiendelea kujaribu
kutekeleza amri ya mama yake, kisha kuzimia na kufariki dunia.
Mama huyo alidaiwa kutumia mafuta maalumu kuuchoma
moto mwili wa mwanaye huyo, ambapo watoa huduma za dharura awali
waliamini kwamba aliuawa kwenye ajali ya moto iliyotokea katika nyumba
ya familia huko nyumbani kwao, Welsh.
Uchunguzi wa awali wa mwili wa mtoto huyo ulibaini
kwamba alifariki dunia kabla ya kutokea kwa moto huo na alikuwa na
majeraha kadhaa ya ndani kwenye mwili wake ikiwemo kuvunjika mbavu, kuwa
na mpasuko kwenue mfupa wa mkono na kuvunjika kidole.
Katika mapitio ya kesi hiyo yaliyochapishwa baada
ya Ege kuhukumiwa kifungo hicho, mmoja wa wafanyakazi kwenye Shule ya
Msingi Yaseen alieleza kwamba aliwahi kushuhudia matukio zaidi ya mawili
ya mtoto huyo kufika shuleni akiwa na majeraha yanayoonyesha kuwa
yalitokana na kipigo, lakini walihofia kutoa taarifa polisi.
Baadhi ya majirani zake walieleza kwamba motto
Yaseen alikuwa akipata tabu kwa mateso nyumbani kwao, lakini hawakuwa na
namna ya kumsaidia kwa haraka kutokana na tabia ya mama yake. Mahakama
hiyo ilielezwa kuwa mama huyo, Ege ambaye ni mtaalamu wa Hesabu ambaye
pia aliweza kupata nafasi ya pekee kutokana na uwezo wake wa kukariri
mistari ya Quran Tukufu alipata tabu sana baada ya kuhangaika kutafuta
mtoto kwa muda mrefu.
Mahakama hiyo ilielezwa kwamba kabla ya kuzaliwa
kwa Yaseen, mama huyo alipata misukosuko ya uzazi na kwamba hiyo
ilitokana na kutokuwapo uhusiano mzuri baina yake na mumewe ambaye
alikuwa ni dereva wa taxi, pamoja na mama mkwe wake.
Pamoja na matatizo hayo, Ege alionekana kuwa mama aliyemjali sana mwanawe na aliendelea kuhakikisha kwamba anakua vyema.
Pamoja na matatizo hayo, Ege alionekana kuwa mama aliyemjali sana mwanawe na aliendelea kuhakikisha kwamba anakua vyema.
Hali ilianza kuwa mbaya baada ya wazazi hao
kuwandikisha Yaseen katika shule maalumu kwa ajili ya kujifunza Quran,
ambapo walitaka awe Hafiz, yaani kuwa na kumbukumbu kubwa kichwani
kuhusu mistari ya kitabu hicho, wakitarajia kuwa hali hiyo itarejesha
heshima kwenye afya.
0 comments:
Chapisha Maoni