Jumanne, 2 Julai 2013

AJALI MBAYA YATOKEA MAENEO YA MABIBO EXTERNAL

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZA AJALI
Kama ule usemi usemao hatujui yatakayo tokea kesho, ndicho kilichotoa muda mfupi uliopita majira ya saa moja jioni leo tarehe 02/07/2013, baada ya gari dogo lililokuwa linatokea maeneo ya Ubungo kwenda uelekeo wa Buguruni kumgonga mwenda kwa miguu aliyekuwa anavuka barabara katika maeneo gereji (garage) Maeneo haya ni mara baada ya kituo cha daladala mabibo external, kituo kinachofuata kama unakwenda Buguruni kinaitwa gereji, hapa ndipo ilipotokea ajali hiyo
mtu aliyegongwa hakuweza kufahamika kwa wakati huo na mashuhuda wengi wa ajali hiyo, lakini ni kijana wa kiume mwenye umri kati ya miaka 30 na 22, rangi yake ni mweusi,  na alikuwa amevaa t-shirt nyeupe iliyokuwa na maandishi ya ADIDAS,
kwa hakika maisha yetu wanadamu ni mafupi sana!! tunaweza kuwa na mipango mengi na malengo mazuri sana, lakini mwisho wetu ukawa hivi pasipo hata kutarajia!! ndio maana wale wanao amini juu ya maisha mengine baada ya kifo, wanfundisha na kusema tunapaswa kujiweka tayari kiroho wakati wote





Damu ilimtoka kwa wingi sana mara baada ya ajali katika maeneo ya kichwani, na hapo ilipotokea ajali kuna kivuko cha waendeo kwa miguu!! kwa mtazamo usio na uthibitisho wa daktari, kijana huyo alifariki muda mfupi baada ya ajali. Tunaomba kuchukua nafasi hii kuwakumbusha madereva wote wazingatie sheria za usalama barabarani, hapa ilipotokea ajali kuna kivuko cha waenda kwa miguu na pia kuna kituo cha mabasi (daladala) kwa vyovyote dereva alitakiwa kupungumza mwendo na hata kama pa mtu anavuka angeweza kumwona na kuepusha ajali. Tunaliomba jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani, wasichoke kuwaelimisha madereva juu ya alama za barabarani

11 comments:

  1. hii ni balaa

    JibuFuta
  2. Duh mamaa masikini pengine alikuwa anaenda kutafuta riski Subhanallah!

    JibuFuta
    Majibu
    1. umeona ee dah inatisha..mungu wangu

      Futa
  3. KWA KWELI INATISHA!!? MADEREVA WANATAKIWA WAWE WAANGALIFU WAKIWA BARABARANI,PIA WAZINGATIE SHERIA, BILA HIVYO TUTAANGAMIA KWA AJALI.

    JibuFuta
  4. Hakika apangalo Mola huwa!

    JibuFuta
  5. duh inna lillah

    JibuFuta
  6. maisha ya vijana yanakatishwa..mungu amsamehe

    JibuFuta
  7. Mungu aiweke roho ya marehemu peponi amen.

    JibuFuta
  8. Mungu aiweke roho ya kijana huyu asiye na kosa mahala pema peponi Aamin. Jina la Bwana lihimidiwe.

    JibuFuta
  9. Eneo hili ndili pia alipopata ajali mdogo wangu Godfrey Haule miaka mitatu iliyo pita. kweli inasikitisha sana.

    JibuFuta

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595