Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewasili nchini jana, Ijumaa, Desemba 27, 2013, akitokea New York,
Marekani.
Rais Kikwete amekuwa New York kwa wiki moja kwa shughuli za kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam,
Rais Kikwete amelakiwa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Makamu wa
Rais, Mheshimiwa Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib
Bilal akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Kikwete Mrisho mara baada ya
kumlaki muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York
Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake nchini
Marekani. Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Bwana Ban Ki Moon na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi
ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.
0 comments:
Chapisha Maoni