Alhamisi, 6 Juni 2013

GWAJIMA; MTU NI ROHO


Hii ni siri ambayo wengi wetu hawaifahamu kuwa Mtu si huu mwili bali mtu ni roho. Kama mtu angekuwa mwili, usingesema "mwili wangu unauma". Lakini mtu ni roho inayokaa ndani ya nyumba ya udongo na hiyo nyumba inaitwa mwili. Mtu aweza kuwa ndani ya mwili au nje ya mwili; Ukisoma katika 2Wakorintho 12:2 "namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne; (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui, Mungu ajua)"

Kumbe kuna uwezekano wa mtu kuwa nje ya mwili na bado akabaki kuwa mtu na ule mwili ukafa hadi roho irudi tena. Lakini akitoka ndani ya mwili ule mwili unakufa, Imeandikwa, Yohana 6:63 "roho ndiyo itiayo uzima mwili haufai kitu" kumbe pasipo roho mwili unaitwa maiti, pia biblia inasema Yesu alipokuwa msalabani aliitoa roho yake ndipo mwili ulipokufa, yeye alikuwa Mungu hivyo alikuwa na uwezovwa kuitoa roho yake. Hivyo mtu anapoitwa amefufuka maana yake roho yake imerudi ndani ya mwili wake.

Kumbe ni muhimu kuishi huku ukijua kuwa wewe si mwili bali ni roho, na ndio maana mwili unaweza kukutamanisha mambo mabaya kwasababu wenyewe ni wa hapa duniani na una siku chache sana. Lakini roho ambayo ndio wewe ni wa milele na lazima uishi milele ama mbinguni au jehanamu kwa wale ambao hawajampokea Yesu.

Hamisha mtazamo wako kuhusu mwili na roho ili ujue kuwa wewe ni roho. na wenyeji wako upo mbinguni si hapa duniani.
Mungu anakupenda kusikia neno hili, chukua hatua; hatupambani katika mwili bali katika roho kwa njia ya maombi. Mungu akubariki!!!

-Pastor Josephat Gwajima

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595