Na Agness
Mayagila, Arusha
KITUO
cha Redio cha Kikristo cha Safina, kilichoko Arusha kimefanya kongamano kubwa
la kumlilia Mungu dhidi ya matendo maovu yaliyofanywa zamani wakati Tanzania
inazaliwa.
Kongamano
hilo ambalo lilikuwa la kuhitimisha mfungo wa siku 40, lilifanyika katika
uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mjini Arusha.
Msuya
alisema kwamba, Tanzania inapitia katika mambo magumu kama vile umaskini, matibabu
finyu na watanzania kutofaidi rasrimali za nchi yao kutokana na misingi mibovu
iliyowekwa wakati Tanzania inazaliwa.
“Katika
maisha ya kawaida mtu anapozaliwa kuna kitu anafanyiwa kulingana na mila za
kwao,wengine wanatambikiwa sasa matendo hayo yanawaletea shida baadaye. Tujiulize
Tanzania ilipozaliwa ilifanyiwa nini?”alisema Msuya.
Alibainisha
kuwa, kama mtu anavyozaliwa na kufanyiwa vitu mbalimbali umefika wakati kanisa
na watanzania wajiulize ni kitu gani kilichofanyika wakati nchi hii inazaliwa.
Alibainisha
kwamba ili Nchi ya Tanzania iwe Nchi ambayo kila mtanzania ajivunie ni lazima
ifike mahali pa kila mmoja kutamani na kuamua kuchunguza habari za kuzaliwa kwa
Tanzania ili kuivunja misingi mibovu iliyowekwa na inayoendelea kuwatesa
watanzania
Akinukuu
katika maandiko matakatifu katika kitabu cha Mathayo 1;18 na luka 1;30
alisema habari za kuzaliwa kwa Yesu ziko wazi na kila anayezita atazipata
ambapo aliwataka watanzania kutafuta habari za kuzaliwa kwa Nchi yao
Akitaja
baadhi ya mambo yanayoashiria misingi yake mibovu alizitaja ndoa kwamba mara
nyingi ndoa zinavunjika kwa kuwa misingi yake iliwekwa kwa mizimu,katika eneo
la uchumi wa watanzania alisema kuwa watu walijilaani kuwa wao watabaki katika
hali ya umaskini na kuwa kutajirika kwao ni lazima waulize mizimu na kusema
kwamba elimu nayo iliwekwa chini ya mizimu na kwamba ndio maana elimu ya
Tanzania imekuwa duni
Awali
akifungua kongamano hilo Mkurugenzi wa Radio safina Dr Daniel Lema alisema
kwamba ni lazima kanisa liamue kwa dhati kumtafuta Mungu ili aweze kuiponya
Nchi kwa kuwa Mungu analiangalia kanisa ili aweze kusamehe dhambi na kuponya
nchi
Wakizungumzia
kongamano hilo baadhi ya waumini waliohudhuria uwanjani hapo Elinice Mollel na
Joel Melau walisema kongamano hilo ni zuri kwa kuwa linawakusanya watanzania na
wakristo pamoja na kumtafuta Mungu kwa pamoja ambapo waliutaka uongozi wa
Safina kuendelea kuwakusanya watu pamoja ili waombe kwa pamoja na watu wamjue
Mungu
0 comments:
Chapisha Maoni