Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam,
zimeendelea kuyafanya maeneo mengine kutopitika, miundo mbinu iliyopo
inashindwa kuyafanya maji kutotuama barabarani, magari na waendao kwa miguu
wanapata shida wakati kama huu
Kijana mmoja amejipatia ajira ya kuvusha watu, japo ni ajira
ya muda mfupi, hapa akimvusha mwanamke wa kizungu katika eneo la River side Ubungo, jirani na Hotel ya Lend Mark
Eneo lenye msukosuko huu mkubwa ni eneo dogo sana, sio eneo la kusubiri serikali itoe pesa au ishughulike yenyewe, nadhani watanzania tunapaswa kuwa wazalendo zaidi, tujitume na kufanya mambo kwa faida yetu!! kwanini tusiwajibike kwa kitu kidogo kama hiki? haya ni maeneo ya makazi ya watu, hata kiongozi wa mtaa huo wa river side angeweza kuwashilikisha watu wa mtaa wake wakafanya jambo ambalo lingesaidia kuondoa kero hii ya maji na mafuriko haya. au tunasubiri mbunge au wizara husika!! TWAWEZA, chukua hatua kujenga nchi yako, usisubiri hadi uwe Rais au mbunge, onyesha uzalendo wak sasa.
GARI LIKIWA LIMEKWAMA KUTOKANA NA MAJI MENGI ENEO LA RIVER SIDE UBUNGO
0 comments:
Chapisha Maoni