WANAWAKE wawili mjini Musoma mkoani Mara, wamejinyonga katika maeneo
tofauti kwa kutumia mkanda wa suruali na mwingine akijinyonga kwa
kutumia mtandio wa nguo yake. Katika tukio la kwanza, Rudia Kyango (40),
mkazi wa Kata ya Kigera, amekutwa amefariki dunia baada ya kujinyonga
kwa kutumia mkanda wa suruali.
Tukio hilo, lilitokea usiku wa kuamkia Aprili 13, mwaka huu ambapo marehemu alijinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali na kufariki dunia.
Baada ya wakazi wa eneo hilo kufika nyumbani kwa marehemu, walitoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi Kigera.
Polisi walichukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya Mkoa wa Mara.
Wakati huo huo, mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Bhoke au mama Marwa, mkazi wa Mtaa wa Ghandhi anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 27 hadi 30, amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio wa nguo yake akiwa chumbani.
Tukio hilo, limetokea juzi asubuhi katika mtaa wa Indra Ghandi, baada ya watoto wake kwenda shuleni.
Majirani walisema, huenda mwanamke huyo alichukua maamuzi hayo, baada ya watoto wake kwenda shuleni na kubaki peke yake nyumbani.
Marehemu kabla ya kifo chake, alikuwa anafanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Mara.
Jeshi la Polisi mkoani hapa, limethibitisha kutokea kwa matukio hayo.

0 comments:
Chapisha Maoni