Jumanne, 23 Aprili 2013

BUNGE UFARANSA LAPITISHA NDOA ZA JINSIA MOJA,

Ni wale tu wanaopenda demokrasia ndio wako hapa, Rais wa bunge la Ufaransa alisikika akisema kwa satui ya ukali wakati wa kupiga kura, ambapo vurugu zilianza kutimka kutokana na kugawanyika wka mawazo ya wabunge hao, huku kinara wao akiwa amevalia nguo za rangi ya pink, rangi ambayo imeasiliwa na wanaopinga vitendo vya ushoga nchini humo.

Kura 331 za kukubali kati ya zile 225 za kupinga kupitisha kwa sheria hiyo ndizo zilizopelekea taifa la Ufaransa kuwa taifa la 14 duniani kuidhinisha vitendo hivyo, licha ya upinzani mkubwa ambao hutokea mara kwa mara nchini humo, ikiwemo leo bungeni.


Waziri wa haki nchini Ufaransa, Bi. Christiane Taubira akihutubia wabunge  wakati wa  maswali kwa serikali, kwenye baraza kuu jijini Paris. © AP
Kutokana na kuchukizwa kwa baadhi ya wananchi kufuatia mpango wa serikali wa kuidhinisha muswada huo, hali ya usalama kwa baadhi ya watu wanaojihusisha na tabia hizo wamekuwa wakipata vitisho kutoka kwa wanaharakati na wananchi wanaopinga, huku kinara mmojawapo wa kuunga mkono vitendo hivyo akipokea barua jumatatu iliyo na unga wa silaha (gun powder), ikiwa ni ishara ya kumtahadharisha aachane na mambo yake vinginevyo atadhuriwa.

Katika hatua nyingine, mshabiki mkubwa wa ndoa za jinsia moja nchini humo amekuwa waziri wa haki, Bi Taubira, ambaye amesema kuwa anaamini ndoa za kwanza kwanza zitakuwa mnamo mwezi juni, hali ambayo italeta hamasa na kubadilisha upeo wa baadhi ya watu wanaipinga vitendo hivyo.

"Naamini wale wanaopinga watajawa na furaha pale ambapo ndoa hizo zinafungwa, ndugu, jamaa na familia wakishuhudia." Bi Taubira anasema.

Wakati rais François Hollande alipoahidi kushughulikia kuruhusu ndoa za jinsia moja, haikuwa na utata kwa sana, lakini jambo hilo limekuwa likimgusa karibu kila mtu, na kupelekea umaarufu wa rais Hollande kushuka sana.

wabunge wa chama cha msimao mkali cha UMP, kupitia mbunge wake, Laurent Wauquire, ameiambia serikali kuwa licha ya wao kuforce kupitisha jambo hilo kuwa sheria, lakini hiyo haitowazuia watu kuingia mtaani na kuandamana kulipinga jambo hilo, wakitaka lirudishwe kwenye hatua ya muswada ili baadae liondolewe kabisa.

Hali yamtaani karibu na bunge ilikuwa tofauti, watu kadhaa wakishuhudiwa kuwa na chupa za wine na champagne, wakijipongeza kwa kunywa, akili zao zikichangamka kwa kujua kwamba sasa wanaweza kuoana jinsia moja na pia kuasili mtoto kama ambavyo haki hiyo ipo kwa wanandoa wowote wale.

Kwa upande mwingine, wapinzani wa ndoa za jinsia moja nao pia walionekana mtaani wakipinga hatua hiyo huku wakionesha alama ya vidole viwili kwenye maeneo mengi akama ambavyo GK imeshuhudia kwenye vyombo kadhaa vya habari.
Mwezi Aprili unashuhudia nchi ya pili ikipitisha muswada huu, huku New Zealand likiwa taifa la kwanza Asia Pacific kuruhusu ndoa za jinsia moja, ikiungana na mataifa mengine ya Ulaya kama vile Uholanzi, Ubeljiji, Spain, Norway, Denmark, Ureno, Iceland na Sweden, ambayo kwa muda sasa imekuwa kimbilio la Waafrika wanaounga mkono ndoa za namna hiyo, huku wakitimkia hukokufunga ndoa zao. Na iwapo Rais wa Ufaransa atatia saini kwenye muswada huo, basi Wafaransa watakuwa wamepewashiwa taa ya kijani kwa ajili ya vitendo hivyo
 HAPA CHINI NI WANAHARAKATI WA NDOA ZA JINSIA MOJO, WAKISHANGILIA KWA MVINYO MARA BAADA YA BUNGE KUPITISHA SHERIA YA NDOA ZA JINSIA MOJA

0 comments:

Chapisha Maoni

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595