Jumanne, 23 Aprili 2013

ASKOFU VALENTINO MOKIWA AWASHUKIA WABUNGE WATOVU WA NIDHAMU

Askofu Dkt. Valentino  Mokiwa.
Matukio yanayoendelea bungeni ikiwemo kutoleana kauli chafu, zimegusa sehemu kubwa ya wananchi, ikwemo vuongozi mbalimbali. Askofu Dkt. Valentino Mokiwa amekuwa mmojawapo kati ya wananchi walioguswa, na kueleka kutoa onyo kwa wabunge wakati akihojiwa na kutuo cha TV cha jijini Dar es Salaam cha Channel 10.
Dkt. Valentino Mokiwa amesema kuwa kutokana na tabia zile, basi ni lazima kuwe na sheria ngumu sana za kuwabana ili ieleweke wazi anaingia bungeni kufanya nini, vinginevyo atakuwa hafai kwa wananchi.
"Yale yanayofanyika kwangu mimi ni magumu sana, ni  sawa na padri au shekhe atukane altarani, sio sawasawa". Anasema Askofu Mokiwa
Aidha pia amewataka wananchi kutopoteza muda kujadili na kufanya mambo yasiyo na maendeleo kwao na badala yake watafute ufumbuzi mambo kama tatizo la maji na elimu.

Hivi karibuni bungeni kumekuwa na kauli chafu na lugha za matusi kutoka kwa baadhi ya wabunge, zikiwemo kauli kama; 'siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa', kejeli kuhusu ujauzito wa wabunge, na hata matusi yasiyoweza kuandikika kwenye vyombo vya habari 

Na kwa namna mambo yanavyoenda, basi ni dhahiri viongozi wetu wanatakiwa kumrejea Mungu na kujawa na hofu yake, huku wakimgeukia Roho Mtakatifu katika maisha yao, la sivyo nchi ndo inaelekea kubaya zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595