Ijumaa, 19 Aprili 2013

SEMINA YA KUONGEZA VIRUTUBISHO KWENYE CHAKULA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Semina ya kuongeza virutubisho kwenye chakula ili kukifanya chakula kiwe bora kwa afya na kukuza kinga ya mwili. Semina iliendeshwa tar 18 - 19/04/2013 na ilimalizika kwa ushindi mkubwa sana katika ukumbi wa Land mark Hotel. LENGO LA SEMINA HII LILIKUWA NI;
Ushawishi
(Persuasion stage
1.Uelimishaji – viongozi mbalimbali wa kisiasa na kidini, waandishi wa habari, wafanyabiashara wakubwa
na wadogo, asasi zisizo za kiserikali, waatalamu wa vyakula na lishe,wahudumu wa afya. nk
2.Shughuli za ushawishi – mashuleni, kliniki, maigizo na ngoma zenye ujumbe ,
sehemu zenye mkusanyiko mkubwa wa jamii husika.
Uhamasishaji
•Kutambulisha Nembo (logo) kwenye jamii.
•Kuhamasisha ulaji wa vyakula vilivyo ongezewa virutubishi/ kuulizia vyakula hivyo
 Ushawishi
 •Kuelimisha jamii yetu juu ya faida za ulaji wa vyakula vilivyo ongezewa virutubishi.
• Kuendelea kuulizia vyakula hivyo
Hatua ya Pili.
Lengo kuu katika hatua hii ni kuelimisha jamii yetu juu ya faida na umuhimu wa kula vyakula vilivyo ongezewa virutubishi,wakati huo huo kuelimisha jamii jinsi ya kutambua Nembo (logo) kwenye vyakula vilivyo ongezewa virutubishi.

Uongezaji virutubishi kwenye vyakula ni njia mojawapo ya kuongeza kiwango cha vitamini na/au madini kwenye vyakula vikuu ili kuongeza ubora wake na hatimaye kuboresha afya ya mlaji kwa nia ya kuzuia au kutibu matatizo ya kilishe yanayotokana upungufu wa virutubishi fulani muhimu mwilini, kama vile vitamini A, madini chuma, na madini joto.
  Majukumu ya Serikali
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni moja ya mdau muhimu katika mradi huu 
Majukumu muhimu ya Serikali katika mpango huu ni pamoja na:- 
Kuhakikisha kuwa kuna mfumo wa kisheria wa usimamizi wa Mapngo 
Kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango 
Kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo uongezaji vrutubishi.

Katika Mpango wa Uongezaji Virutubishi kwenye Vyakula, Serikali hutekeleza majukumu yake Wizara na Taasisi mbalimbali
Wajibu Wenu 
Kufanikisha kufanikiwa kwa kampeni hii katika ngazi za wilaya na vijiji.
•Wawakilishi wa kampeni hii katika eneo lako.
•Kujibu hoja zinazopinga kampeni hii katika eneo lako
•Kuelimisha na kushawishi jamii inayokuzunguka
•Kuripoti matukio yanayoweza kusababisha kupunguza mafanikio ya kampeni hii.
Kwa mawasiliano zaidi kuhusu elimu hii piga:-
0712 471637
0787 440752   
0783 100896

0 comments:

Chapisha Maoni

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595