hivi sasa kuna tuzo furani inashindaniwa na waimbaji mbalimbali, kutoka nchi za kiafrica ijulikanayo Africa Gospel Music Awards(AGMA), sasa fuatana na mwandishi aliyeandika habari hizi kutoka chombo kimoja wapo cha habari, na uweze kutazama zaidi kiroho juu ya mashindano hayo:-
Martha Mwaipaja nyota yake imeonekana kung'ara na kutambulika kimataifa baada ya kupendekezwa kwa mara ya kwanza kuwania tuzo za injili za Afrika ziitwazo Africa Gospel Music Awards(AGMA) ambazo zinatarajiwa kutolewa mapema mwezi wa saba mwaka huu jijini London.
Mwimbaji huyo anayetamba na album yake ya pili aliyoitoa mapema mwaka jana amewekwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya mwimbaji wa mwaka Afrika mashariki akiwa sambamba na nyota mwingine wa muziki wa injili nchini Christina Shusho ambaye amependekezwa kuwania tuzo hizo kwa mara ya tatu mfululizo. Waimbaji hawa pekee kutoka Tanzania watakuwa wanawania tuzo hiyo na waimbaji wengine kutoka Kenya na Uganda.
nchini, ukiwa kama Mtanzania na mwana Afrika Mashariki tunaomba chukua muda wako wa dakika zisizopungua tano kuwapigia kura waimbaji wetu.
Wanaowania tuzo ya mwimbaji wa mwaka Afrika mashariki ndio hawa
Eunice Njeri (Kenya)
Christina Shusho(Tanzania)
Jimmy Gait (Kenya)
Kambua (Kenya)
Jackie Senyonjo(Uganda)
Kris Eh Baba (Kenya)
Coopy Bly-Uganda
Martha Mwaipaja-Tanzania
DK Kwenye Beat(Kenya)
Eko Dydda(Kenya)
Hata hivyo katika tuzo hizo kama ilivyokawaida waimbaji kutoka nchini Kenya wameonekana kung'ara katika kuwania tuzo tofauti huku, kinyang'anyiro kikali kinategemewa kuwa kusini mwa bara la Afrika ambako waimbaji nyota wa Afrika ya kusini wanawania tuzo hizo pia. Ambapo katika kinyang'anyiro hicho mwimbaji nyota kutoka kundi la Joyous Celebration Charisma Hanekam anatarajiwa kuwa mmoja wa waimbaji siku ya kutolewa kwa tuzo hizo zitakazofanyika tarehe 6/7/2013 katika ukumbi wa The Great Hall, Queen Mary jijini London nchini Uingereza.