DUNIA KUNA MAMBO YA KILA AINA, YA AJABU NA MENGINE YA KUSHANGAZA KWA MTU AMBAYE NI MARA YAKE YA KWANZA KUSIKIA AU ASIYE AU IMANI FURANI, ANGALIA IBADA HII HUKO INDIA
Sherehe ya kuoga Uchi katika Mto Ganges yaanza leo
Waumini wa dini ya Kihindu wakienda kuoga ili kujitakasa na dhambi walizotenda
Mamilioni ya Wahindu wakiwa wamejipaka majivu tayari kuingia mtoni kuoga
Waumini wa dini ya Kihindu wakishangilia baada ya kuosha dhambi zao mtoni
Msichana wa Kihindu akioga kuondoa dhambi
Baba akimwogesha wanae
Waumini wa Kihindu wakisali kwa Uchaji mkubwa
Akina mama nao huchanganyika na wanaume wakati huo wa kutakasa dhambi zao kwa maji
Makuhani wa wakiongoza ibada
Inatarajia hadi leo usiku watu milioni 11 watakuwa wameoga
Baada ya kuoga wateule hubeba maji kwenye vyungu vya vyuma kupeleka mahekaluni
Mamilioni ya watu wanafurika usiku na mchana. Utakaso huu huchukua siku 55 hivyo umeanza leo na kumalizika March 5
Kutokana na wingi wa watu, treni kama unavyoona zinakuwa zimepakia hadi
dereva hapati pa kuangalizia. Kila penye upenyo panakaa mtu isipokuwa tu
kwenye magurudumu
Hii ni treni ya umeme ambamo watu wameshindwa kupanda juu lakini pembeni wamenyomi
ALLAHABAD, India,
Mamilioni ya wai wa dini ya Hindu leo Jumatatu wameanza hija yao ya
kuoga katika makutano ya mito mitatu ya Ganges, Yamuna na Saraswati
inapokutana. Kwa mujibu wa Imani ya Kihindu, binadamu anakuwa ametenda
dhambi nyingi katika mzunguko wa mwaka na hivyo anahitaji kutakaswa na
dhambi zake. Waumini wanaume wanajipaka majivu kuanzia utosini hadi
unyayo na mara nyingi wanakuwa uchi wa mnyama ingawa sikuhizi wengine
wanapendelea kuvaa pajama, wanaingia kwenye mto huo na kuoga nakuamini
kuwa wameondolewa dhambi zao zote na nuksi nyingine zote.
Hii ni sherehe kubwa na inayodumu muda mrefu kuliko zote duniani kwani
inadumu kwa kipindi cha siku 55, hivyzia leo hadi tarehe 10 marrcdu
watakuwa katika sherehe hizo.
Mratibu mkuu wa sherehe hizo Mani Prasad Mishra amesema karibu watu milioni 3 walikuwa wameshaoga leo asubuhi na watu wengine milioni 11 wanatarajiwa kuoga hadi jioni ya leo.
Zaidi ya watu milioni 110 wanatarajiwa kuoga kwenye eneo hilo liitwalo
SANGAM. Hili ni eneo ambapo makutano ya mito ya GANGES, YAMUNA
NASARASWATI . Sikukuu hii inatelemea mwonekano wa nyota zinazolandana
angani. Baada ya nyota hizo kukaa katika mkao fulani basi wahindu
wanaenda kuoga ili kujitakasa na madhambi yao na kuopuka kufo na
kuzaliwa upya katika hali ya adhabu.
Soma kwa kirefu zaidi hapa: http://www.bbc.co.uk/news/world-asia-india-21006259
0 comments:
Chapisha Maoni