Singida. Mama Mzazi wa Mkuu wa Polisi nchini
(IGP), Ernest Mangu, Mwanaidi Msengi, amemsihi mwanawe kufanya kazi kwa
bidii asimwangushe Rais Jakaya Kikwete ili asije kujutia kumpa nafasi
hiyo.
Mwanaidi alisema licha ya furaha kubwa aliyonayo,
anamuasa mtoto wake kuchapa kazi kwa bidii kama njia mojawapo ya
shukurani kwa Rais Kikwete kwa kumteua akiwa mwenyeji wa kwanza kutoka
Mkoa wa Singida kushika wadhifa huo nyeti.
“Hii ni heshima kubwa sana kwangu binafsi, ndugu
zake, wakazi wa Kijiji cha Kihunadi na Mkoa wa Singida, kwa hiyo lengo
langu ni kumwombea mtoto wangu Mangu asimwangushe Rais... Eee Baba
(Mungu) msaidie mwanangu atimize wajibu wake ipasavyo ili Rais Kikwete
siku moja aseme hakukosea kumpa Mangu ukuu wa polisi,” alisema Mwanaidi.
Juzi ndugu, jamaa na marafiki walifanya hafla
ndogo iliyoambatana na vifijo, nderemo na bashasha na wakazi wa Kijiji
cha Kihunadi, Tarafa ya Ilongero, mkoani Singida, alikozaliwa IGP huyo
huku wakidai sasa kijiji chao kitajulikana haraka ndani na nje ya
Tanzania.
Walisema licha ya kujulikana, changamoto
mbalimbali zinazokikabili kijiji hicho zitapatiwa ufumbuzi wa kudumu
mapema iwezekanavyo.
Mwanaidi alisema Mangu alianza kumwonyesha
mafanikio tangu Shule ya Msingi Kinyagigi, kwani alikuwa na bidii ya
kujisomea mara kwa mara alishika nafasi ya kwanza au ya pili.
Kwa mujibu wa Mwanaidi, IGP Mangu ni mtoto wa pili kati ya saba aliowazaa.
“Mangu ni wa pili kati ya watoto wangu saba baada
ya kuolewa na baba yao, Jumbe Omari Mangu aliyefariki Aprili 27, 1988.
Jina la Jumbe linatokana na kupewa kazi ya ujumbe wa wakoloni wakati wa
ujana wake,” alisema.
Wenyeji wa kijiji hicho, walisema wamekuwa
wakiamini Mangu atafika mbali kwa kushika nafasi za juu za uongozi,
kutokana na uadilifu, uchapaji kazi, ukaribu wake na wananchi, uaminifu
na uwazi.
Mwanaidi alisema Mangu alipofaulu kwenda sekondari
alilazimika kuomba ng’ombe kwa mke mweza, ili akamuuze apate fedha za
kugharimia masomo ya mtoto wake.
“Mke mwenzangu alimtoa ng’ombe wake, lakini Mangu
alipomuuza kwenye mnada pale Singida mjini, aliibiwa fedha zote na
alirudi nyumbani akilia sana,” alisema.
Alisema baada ya hapo alimwambia mtoto wake
kwamba, ataanza kutengeneza vyungu kwa kutumia udongo wa mfinyanzi ili
kupata fedha za kugharimia masomo yake. “Nashukuru Mangu alinielewa vizuri kwa sababu alishiriki kubeba kichwani
vyungu hivyo wakati wa kuviuza hadi kichwa chake kilikaribia kuwa
kipara. Nilibuni chanzo kingine cha mapato ambacho kilikuwa ni kukoroga
na kuuza pombe za kienyeji,” alisema. Inadaiwa baba yake, IGP Mangu
alioa wanawake sita kwa nyakati tofauti, lengo likiwa ni kupata mtoto wa
kiume. Wengi wa wake zake walikuwa wakizaa watoto wa kike
Maoni haya yameondolewa na mwandishi.
JibuFutaMaoni haya yameondolewa na mwandishi.
JibuFutaMaisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma
JibuFutaKwaheri Gerd Ulrich