KANISA la EAGT hivi karibuni lilimtunuku tuzo Mkurugenzi wa makampuni ya Msama Promotions kwa kutambua mchango wake katika uchangiaji wa maendeleo ya jamii.
Akizungumza baada ya
kukabidhi tuzo hiyo, juzi Askofu Philemon Phiri wa jimbo la Mikocheni
akimwakilisha Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Moses Kulola
alisema tuzo hiyo kwa Msama ni utambuzi wa anayoyafanya katika kusaidia jamii.
alisema tuzo hiyo kwa Msama ni utambuzi wa anayoyafanya katika kusaidia jamii.
Askofu Phiri alitumia fursa hiyo
kumpongeza Msama kwa uandaaji wake bora wa matamasha ya Pasaka na
kueleza kuwa mungu amempa ufunuo ambao ni endelevu.
Naye Msama alishukuru tuzo hiyo na kueleza kwamba tamasha la Pasaka litaendelea kila leo tena kimataifa zaidi hadi duniani.
Katika hatua nyingine mwimbaji
nguli wa muziki wa Injili wa Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi nchini Kenya, amesema atatumia
tamasha la pasaka kutambulisha wimbo wake wa Kiti Chako uliopo kwenye
albamu yake mpya ya Sifa za Mungu.
Akizungumza na Pata Habari,
baada ya kuwasili kutoka nchini Kenya kwa ajili ya kuhudhuria tamasha la
pasaka linalotarajiwa kufanyika Jumapili hii katika uwanja wa taifa
jijini Dar es Salaam alisema, atautambulisha wimbo huo ambao una ujumbe
mzito wa neno la mungu.
Kwa mujibu wa Mukubwa albamu
yake hiyo ni zaidi ya nyingine alizowahi kurekodi hii kwa sababu ameimba
ushuhuda wa maisha yake baada ya kupata matatizo ya kukatwa mkono
wake.
“Nashukuru kupata tena nafasi
ya kuwa mmoja wa waimbaji kwenye tamasha la mwaka huu, nimejiandaa vya
kutosha mashabiki wafike kwa wingi kupata ujumbe mzito wa neno la mungu
pia nitatambulisha wimbo wangu mpya siku hiyo” alisema Mkukubwa.
Alisema albamu yake hiyo
inanyimbo saba, ambazo ni Kiti chako, Shukrani ya punda, Nitaishi
wakitazama, Habari njema, raha yangu, sijafika, Sifa za mungu,
Nimewasamehe wote.
Kwa upande wa Faraja Ntaboba,
alisema kauli mbiu ya tamasha la pasaka la mwaka huu inayosema kuwa
‘Amani na Upendo’ imempa moyo sana, inagusa Afrika nzima kwa kuwa kuna
watu wanalia kwa kupoteza amani.
Aidha mwimbaji huyo alitoa
wito kwa mashabiki wa tamasha hilo linalotarajia kufanyika mikoa
mitano, kuwa wasisherehekea tu bali waje wakijua amani inatafutwa,
aliahidi kufanya mambo makubwa siku ya Jumapili.
Tamasha la Pasaka litafanyika Dar
es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine
Mbeya, wakati Aprili 3 Uwanja wa Samora mkoani Iringa na Aprili 6 Uwanja
wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba,
Mwanza.
0 comments:
Chapisha Maoni