Amesema karama za Roho Mtakatifu ni zawadi au urithi wetu kama kanisa kutoka kwa Mungu, na ndio maana Yesu alisema nawaleteeni ahadi ya Baba, kwahiyo ili mtu awe safi mbele za Mungu, cha kwanza ni kupatana na Mungu kwa kutubu dhambi na baada ya hapo anapokea kipawa cha Roho Mtakatifu, kitakuwa juu yako kama utaelewa kuwa ni urithi wako na ahadi ya Mungu kwetu
Na ndiyo maana Roho Mtakatifu anatajwa tangu kitabu cha Mwanzo hadi ufunuo wa Yohona, mchungaji anasema katika ujumbe kwa kanisa leo kwamba, wakati wa Musa, Samsoni, Daudi Yoeli nk utaona Roho Mtakatifu anatajwa kutendakazi na watumishi hao wa Mungu.
huu ni ujumbe mfupi kwako unaoletwa kwako kila jumapili, tunaomba utfakali na uchukue hatua kwa kuwa lipo kusudi la Mungu kwako kupitia ujumbe huu ulioletwa na mchungaji Mwanibugu. ubarikiwe sana unapoendelea kutafakari ujumbe huu wa leo