Mtumishi wa Mungu, ambaye amejaliwa karama ya uimbaji Vaileth Mwaisumo, atafanya uzinduzi wa Albam yake tarehe 9/6/2013 katika ukumbi wa kkkt uliopo barabara ya Arusha, shughuli hiyo itafanyika kuanzia saa nane mchana katika siku hiyo ya Jumapili, Vaileth Mwaisumo atafanya shughuli hiyo akisindikizwa na kwaya mbalimbali pamoja na waimbaji wengine wengi, kama vile kwaya ya Sayuni band, Lutheran Ipagala kwaya, Capital kwaya, kwaya kutoka chuo kikuu cha Dodoma nk, na waimbaji wengine wa kujitegemea atakuwepo pia tulibako Mwakasege, Velian Makabala, Matlida na wengineo
Kwa kuwa uimbaji wa dada Vaileth Mwaisumo umekuwa ukiwagusa wengi, taarifa zilizotufikia sauti ya kanisa ni kwamba, mgeni rasmi atakaye shiriki katika uzinduzi huo ni mkuu wa mkoa wa Dodoma mheshimiwa Nchimbi, kwa hakika itakuwa siku ya kipekee sana!!
watu wote wenye mapenzi mema mnaombwa kushiriki katika tukio hilo muhimu, na zaidi maombi yanahitajika sana kwa kusudi la kufanikisha huduma hiyo.
Jumatatu, 27 Mei 2013
UZINDUZI WA ALBAM MPYA YA NYIMBO ZA INJILI UNAFANYIKA DODOMA TAREHE 9 JUNE 2013
Posted By:
Unknown
On 09:55
In
Call Us Now:
+255 655 732121,
+255 716 758595 / +255 762 758595