Jumanne, 28 Mei 2013

MAKUMI ELFU WAANDAMANA UFARANSA KUPINGA NDOA ZA JINSIA MOJA, MABOMU YARINDIMA

Watu zaidi ya 100 wamekamatwa katika maandamano ya kupinga ndoa za watu wa jinsia moja, ambayo yalifanyika mjini Paris na takribani watu laki 1 na 50 walishiriki katika maandamano hayo, kuonyesha hasira waliyo nayo juu ya sheria inayoruhusu ndoa hizo ambayo ilitiwa saini na rais François Hollande wiki iliyopita.
 Makumi elfu ya waandamanaji wakiwa wamekusanyika jijini Paris
 Mchungaji mmojawapo jijini Paris naye akishiriki maandamano hayo


Sheria hiyo ambayo vile vile inaruhusu mashoga kuasili watoto, ilipitishwa baada ya malumbano makali juu ya suala hilo ambapo Maandamano hayo yalianzia katika vituo mbali mbali mjini humo, na kukutana katikati ya mji.
Aidha Waandamanaji walitaka sheria hiyo iondolewe, na kuapa kuendelea kutetea umuhimu wa kile walichokiita haki ya mtoto kuwa na familia, kupitia mama mmoja na baba mmoja, tofauti na sheria hiyo inayoruhusu mtoto kulelewa na nyumba yenye wapensi wa jinsi moja.
Hata hivyo Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wanaharakati wa kikundi chenye msimamo mkali wa kizalendo.
 Waandamanaji wakijipanga namna ya kukabiliana na polisi

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595