Jumanne, 4 Juni 2013

MANABII NA MAASKOFU WANAOTUMIA MAJI NA MAFUTA NI MATAPELI


Askofu mkuu na mwanzilishi wa kanisa la Redeemed Gospel Church Dunia Askofu Arthur Kitoga amesema viongozi wa kanisa lolote wanaotumia mafuta au maji yanayoitwa maji ya upako au mafuta ya upako kwenye huduma za maombezi, amesema wanayoyatumia ni kwa kuwatapeli waumini kwa kuwajengea matumaini ya uongo katika maisha yao, amesema anasikitishwa sana kwa kuibuka watu leo ndani ya kanisa na kuanza kudai eti kuna mafuta na maji ya upako yanayo leta baraka na uponyaji, hii sio sahii kibiblia
Askofu Kitoga aliyasema hayo wakati wa mahafali ya wahitimu wa chuo cha watumishi cha Hope For The Nation Bible Centre kilichopo jijini Dar es salaam
Askofu Kitonga, aliwataka mahitimu hao kwenda kutumika kwa uaminifu sawa sawa na Neno la Mungu linavyo wataka kufanya, iweni wanyenyekevu wakati wote ili mkaibadili jamii ipate kumjua Mungu, niwambie kitu ambacho nimekuwa nakisema mara nyingi, wengi wanaitwa lakini wateule ni wachache, leo tuna mbuzi wengi kuliko kondoo, je tutawajuaje hao kondoo, tutawatambua kwa jinsi wanavyofuata maandiko na jinsi wanavyo tumia madhabahu, Watanzania msijitenge na Neno la Mungu, leo kuna walimu wauongo kila kona wanawauzia watu mafuta na maji madhabahuni kwa kuwaambia watu eti yana upako!! hii ni ajabu sana. wameanza kuuza na mifagio eti ya kumfagia shetani, ndugu zangu tafakalini Neno la Mungu kwa makini ndipo mtakapo fanikiwa

Wengine wanakwenda Israeli na kuja na mchanga au udongo na kuwauzia watu kwa kuwambia watu kwamba udongo huo umebalikiwa na unanguvu za Mungu, je hii imeandikwa wapi katika Biblia?

Askofu Kitonga alizungumzia pia uhusiano wa watumish wa Mungu kuwa sio mzuri kati ya kanisa moja na jingine, na akasema yeye ni rais wa muungano wa makanisa ya kievanjelistiki katika Africa kwa upandea wa mashariki, lengo la umoja huo ni kuyaleta makanisa yote katika umoja ili yawe kitu kimoja, wito wangu ni kwamba, watumishi wote tuungane na tufanye kazi pamoja sawa na Neno linavyosema katika Yohana 17:21
 Alisema tatizo mojawapo linalowafanya watu washindwi kuwa kitu kimoja, wengi wanajiinua sana, hakuna unyenyekevu ndani mwo kama alivyokuwa Musa, wengi wanajiinua kwasababu ya vyeo na uwezo wao kipesa, lakini maandiko yanasema katika kitabu cha Mithali 16:18 kiburi hutangulia uangamivu na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko, mtumishi wa Mungu Bonnke anakuja, nawaomba wote kwa pamoja tukutane pale na tukafanye toba kabla ya anguko na aliyeanguka kwasababu ya kiburi Bwana atamsamehe na kumwinua tena

Askofu Kitonga amekemea kitendo cha Watumishi wa Mungu kuwaachia wanasiasa madhabahu, amesema ili ni jambo baya sana kiroho, mnawapa madhabahu badala ya kukemea matendo maovu wanayofanya? mnataka wawape kitu gani hao cha kiroho, kama wanakuja ni vizuri, lakini waje kwa lengo la kuombewa na kupata ushauri kiroho na sio kupewa nafasi katika madhabahu ya Bwana, wahubiri wa Injili tusigeze Injili kuwa intertainment au burudani, kwanini mnataka kuharibu kazi ya Mungu kwa kiwango cha kutisha kiasi hiki? watumishi wenzenu wakija kwenu mbona hawapewi madhabahu, lakini akiingia mwana siasa moja kwa moja madhabahuni. hii inaonyesha ni jinsi gani mnavyotafuta pesa na sio ufalme wa Mungu alisema Askofu

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595