Akijibu swali alisema, aliyepaswa kujibu swali hili ni Rais Kikwete kwakuwa yeye ndiye anayeshughulikia migogoro ya nchi za maziwa makuu. Hata hivyo alimtaka Rais Kikwete kukaa na Rais Kabila na kuangalia ni jinsi gani wanavyoweza kuondokana na hali hiyo nchini Congo na hasa ukizingatia kwamba migogoro Congo DRC inatokana na maslahi, huo ulikuwa mkutano wa kwanza wa Rais Obama na waandishi wa habari wa ndani na nje katika ziara yake hapa nchini Tanzania.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na
mgeni wake Mama Michelle Obama muda mfupi baada ya kuwasili kwa Rais
Obama nchini kwa ziara ya siku mbili nchini.
Mapokezi ya Rais Obama na mkewe Michelle yalivyokuwa mara baada ya kuwasili ikulu jijini Dar es salaam, ilikuwa na shangwe na vigelegele
Rais Obama akipanda mti aina ya mpingo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo
0 comments:
Chapisha Maoni