Alhamisi, 27 Juni 2013

WASOMI DODOMA WAMEMWOMBA LOWASSA AGOMBEE URAIS 2015

Dodoma. Wanafunzi zaidi ya 600 wanaosoma Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) ambao walimaliza elimu yao ya Sekondari katika shule za Kata nchini, wamemuomba Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Wawakilishi wa wanafunzi hao wapatao 40,juzi jioni walimtembelea kiongozi huyo nyumbani kwake maeneo ya Area C mjini hapa na kula naye chakula cha usiku, huku wakimueleza kuwa wapo tayari kumpigia debe, kumchangia fedha za kuchukua fomu pamoja na kuwashawishi vijana wenzao kwamba Lowassa ndiye kiongozi anayefaa kwa sasa.Hafla hiyo pia illihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanafunzi hao.

1 comments:

  1. hivi watanzania tuna akili kweli? yaani pamoja na kujiudhuru sababu ya wizi,bado mnashabikia kwamba awe rais, hiyo ni akili matope!

    JibuFuta

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595