Rais Kikwete ni kiongozi wa aina yake katika uongozi wake,
ni kawaida kwa viongozi wengi hasa wenye ngazi za juu, kutojihusisha na maisha
ya watu wenye maisha ya chini au yakawaida, hali hiyo ya viongozi wengi, ipo
tofauti na jinsi alivyo JK. Kikwete, amekuwa ni mtu wa watu, anayependa
kujihusisha na watu wote bila ubaguzi, na pia amekuwa si mtu anayehusika na
kuwasaidia walio katika umaskini. Mara nyingi utamkuta JK yupo kwenye misiba,
au amekaa chini kwenye mkeka akiwapa pole waliofiwa, au amechuchumaa
akizungumza na mlemavu.
Pia katika utafiti wa makala nyingi, utaweza kugundua
kwamba, Jk Kikwete hana tuhuma za mojamoja zinazo mhusu yeye, kama ni tuhuma,
utazikuta ni zile za watendaji wake tu na sio yeye mwenyewe. Mpaka sasa hakuna
tuhuma yoyote inayomkabiri tangu ashike madaraka ya uongozi wa juu wan chi. Je
tunaweza kumpata kiongozi wa aina hii baada yake? Je kama ni wewe utakaye shika
madaraka ya juu katika nchi yetu, utaweza kuwapenda walemavu na utawakumbatia?
Je utaweza kuongoza bila tuhuma? Je udini hautakuwa sehemu ya maisha yako,
Kikwete ni muislam, lakini hakuna chembe ya udini ndani mwake, hadi waislam
wanasema JK ni Mkristo, kwa jinsi wanavyo mwona msimamo wake, kwani wengi
walitarajia kumwona akiwa na upendeleo na dini yake. Je kama ungekuwa wewe
ungekuwaje? Haya ni maoni yangu na kama utaweza ni vema ukachangia katika maoni
hapa chini.
hakuna lolote
JibuFutakweli jk ni mfano wa kuigwa, wanaokataa na kwasababu zao binafsi lakini si za kijamii
JibuFutanamkubali mzee huyu,mungu amlinde
JibuFutabaada ya jk kuondoka watu watajua thamani yake, maana tutakuja pata viongozi wadini wakutupwa au wakabila, maana viongozi wote wanaoonyesha kugombea urais baada yake wamejikita aidha makanisani au misikitini au kikanda au kiukabila
JibuFutaSI Raisi Binadamu kupata Moyo kama wake.Maana Naweza Sema Upendo Wake Umezidi kwa Wengi. Kuipenda Nchi kama Nyerere.
JibuFutaNi Binadamu Wa kuigwa Ingawa Ni Vigumu kuufikia Upendo Alionao Rais huyu.
JibuFuta