Askofu kakobe yupo hapa Tanzania katika ukimya wa maono makubwa ya kuihubiri Dunia yote, kwa mfano mwezi wa sita mwaka huu 2013 atakuwa nchini Canada kwaajili ya kuwahudumia watu wa nchi hoyo kiroho katika mkutano utakaofanyika katika jiji kubwa la Toronto, kwasasa maandalizi yanaendelea kwa kasi kubwa na watumishi wa Mungu walioko huko ili kufanikisha mkutano huo mkubwa
Lingekuwa jambo jema zaidi kwa wakristo wote kuungana naye kwa kuiombea kazi anayokwenda kuifanya huko, anakwenda kuifnya kazi ya Mungu na siyo yake, ni vema watumishi wa Bwana na watanzania kwa ujumla tumtie moyo ndugu yetu na mtumishi huyo
Ni wakati wa kumtangaza YESU kutokea Tanzania, tumwombe MUNGU hakika atatupa mataifa yote kuwa urithi wetu(ZABURI 2:8)
JibuFuta