*Waasi M23 waua Meja wa JWTZ Kongo
RAIS Jakaya Kikwete amemuomba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, kuwa msuluhishi wa mgogoro
wa chini kwa chini unaoendelea kati ya Tanzania na
Uamuzi huo, ulitangazwa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Pinda alitangaza uamuzi huo, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu ambapo Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alitaka kujua hatua za Serikali katika kile kinachoonekana Tanzania kutaka kutengwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbowe, alisema hatua ya nchi za Rwanda, Kenya na Uganda kuendesha vikao kupitia wakuu wa nchi ikiwemo kujitoa kwa nchi ya Rwanda kutumia Bandari ya Dar es Salaam, kunaashiria mwelekeo mbaya.
Alisema hatua ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujitenga na Tanzania, hali iliyofikia kwa wabunge wa nchi za Rwanda, Uganda kutaka vikao vya Bunge vifanyike kwa mzunguko wakati makao makuu yake yapo mjini Arusha, ni moja ya mambo ambayo yanazua maswali mengi.
Kutokana na swali hilo, Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali haina sababu ya kujenga uhasama na nchi ya Rwanda, kwani nafasi ya Tanzania katika nchi za Maziwa Makuu na Afrika kwa ujumla inatambulika.
Alisema Tanzania kwa muda mrefu, imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuzikomboa nchi za Afrika kupigania uhuru wake na haina sababu ya kugombana na Rwanda.
Hata hivyo, alisema pamoja na kutokea kwa hali hiyo, hakuna asiyejua kuwa Tanzania bado ni kimbilio kubwa la wakimbizi wengi kutoka katika nchi za maziwa makuu.
“Hakuna asiyejua nafasi ya Tanzania hasa kwa nchi za Maziwa Makuu, imekuwa kimbilio la wakimbizi wao wengi. Haiwezekani ushauri uliotolewa na Rais Kikwete ikawa sababu ya kuingia katika mgogoro, kwani katika hili ninaungana na Rais juu ya ushauri wake kwa Rwanda
Kutokana na hali hiyo, Pinda alisema kinachohitajika ni kutatua mgogoro huo kwa busara na tayari Rais Kikwete ameshamuomba Rais Museveni kuwa msuluhishi wa sakata hilo.
“Hatuhitaji kuunda tume ya kufanya usuluhishi wa jambo hili, kinachohitajika zaidi ni busara ili kumaliza suala hili, kama litaendelea tutaangalia jinsi ya kutumia busara zaidi,” alisema Pinda.
Alisema ni wazi ushauri wa Rais Kikwete, umekuwa ukibezwa hata kufikia kutumika vyombo vya habari vya mataifa ya nje kwa kukuza mgogoro.
Alisema mgogoro huo unatokana na Tanzania kutoa ushauri kwa nchi ya Rwanda juu ya kukaa katika meza moja na waasi, ili kuacha mapigano kwa maslahi ya wananchi wa Rwanda.
Alisema mgogoro huo ni kutokana na ushauri wa Rais Kikwete alioutoa katika moja ya mikutano iliyofanyika nchini Ethiopia, kwa kuitaka nchi hiyo kukaa meza moja na waasi wa FDLR.
“Ushauri wa Rais Kikwete kwa Rwanda, umekuwa ukibezwa hali ambayo imefikia hata kwa nchi hiyo kumuona hana nia njema na nchi hiyo. Si kweli hata kidogo.
“Inashangaza kuona wenzetu wa Rwanda kulibeba suala hili kwa nguvu kubwa kiasi cha kuonyesha hali ya kutoelewana, kauli hii ilitolewa kwa nia njema kabisa,” alisema Pinda.
Katika kile kinachoitwa mkakati wa mataifa matatu, Rais wa Rwanda, Paul Kagame juzi aliwasili mjini Mombasa nchini Kenya na kushiriki katika mkakati wa kuzinduliwa kwa gati namba 19 katika bandari ya Mombasa, ambayo inakusudiwa kutumiwa na nchi hizo kupakulia na kusafirishia mizigo yake.
Mbali ya Rais Kagame, uzinduzi wa gati hilo uliwakutanisha pia Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Salva Kiir wa Sudani Kusini na mwenyeji wao Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa viongozi hao wamekuwa wakikutana kwa mwamvuli wa viongozi wa Afrika Mashariki, huku Rais Jakaya Kikwete akitengwa kutokana na ushauri wake kwa Rwanda.
0 comments:
Chapisha Maoni