Jumapili, 14 Aprili 2013

MEJA JENERALI MAKAME AFARIKI, RAIS KIKWETE AOMBOLEZA


Kwa hakika siku zetu zimehesabiwa, kama anavyosema maandiko matakatifu, sisi hapa Duniani ni wapitaji na wasafiri, ndicho kilichotokea kwa mpendwa na kamanda wetu, mtu wa watu, Meja Jenerali Makame,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhesimiwa JK. Kikwete leo hii amepokea taarifa za kuuzunisha juu ya kifo cha aliyekuwa mkuu wa JKT Meja Jenerali mstaafu Rashid Makame kilichotea asubuhi ya leo tarehe 14.4.2013 katika hospitali kuu ya jeshi ya Lugalo
Mbali na kuwa mkuu wa JKT, Meja Jenerali Makame, amelitumikia Taifa kwa nafasi mbalimbali, kama vile mkuu wa mkoa wa Mbeya, nakisha balozi wa Tanzania nchi Malawi.
Kufuatia kifo hicho, Rais amemtumia salamu za rambirambi, mkuu wa majeshi Jenerali Devis Mwamunyange kuomboleza kifo hicho, pia Rais amewatumia maafisa wote wa jeshi salamu hizo kupitia kwa mkuu wa majeshi pamoja na wapiganaji wote.

sisi sauti ya kanisa tunawapo pole wafiwa wote, na pia kumwomba mwenyezi Mungu awajalie faraja na amani wakati mgumu wa kipindi hiki cha msiba, poleni sana watanzania kwa msiba huu Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Mstaafu Makame Rashidi (pichani), ambaye ameaga dunia alfajiri ya leo, Jumapili, Aprili 14, 2013 katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, Dar Es Salaam.

Enzi za uhai wake, mbali na kuwa mkuu wa JKT, Meje Jenerali Makame pia alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Balozi wa Tanzania katika Malawi.

Kufuatia msiba huo, Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange kuomboleza kifo hicho.

Rais Kikwete ameeleza kuwa alimfahamu Jenerali Makame enzi za uhai wake kwa miaka mingi katika utumishi wa umma. Alimfahamu kama mtumishi mtiifu na msikivu ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kama kiongozi mwadilifu na mwaminifu katika nafasi yake ya Ukuu wa Mkoa na kama Mwanadiplomasia mahiri ambaye aliiwakilisha Tanzania nje ya nchi kwa uhodari mkubwa.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Nimepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Meja Jenerali Mstaafu Makame Rashid ambaye nimejulishwa kwa ameaga dunia asubuhi ya leo kwenye Hospitali ya Lugalo. Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo hiki.”

Ameongeza Mheshimiwa Rais Kikwete: “Nakuomba kupitia kwako vile vile unifikishie salamu zangu za rambirambi kwa maofisa wote wa Jeshi letu ambao wameondokewa na ofisa mwenzao na askari wote ambao wameondokewa na kiongozi wao. Aidha, kupitia kwako, naitumia familia ya Marehemu Makame Rashid pole nyingi kwa msiba huu mkubwa wa kuondokewa na mhimili wa familia.”

“Nakuomba uwajulishe kuwa niko nao katika msiba huo mkubwa kwa sababu naelewa huzuni na machungu yao

 




0 comments:

Chapisha Maoni

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595