Kumetokea na tukio la kusikitisha ndani ya kanisa, hii ni baada ya watu wanne kufariki wakiwa katika ibada, wengi utarajia kwamba ndani ya kanisa yupo Mungu ambaye ni mleta mzima na baraka, tukio la vifo hivi lilimetokea ndani ya kanisa la Synqgogue church of all nations nchini Ghana, kanisa ambalo linaongozwa na kasisi Tb Joshua (SCOAN) kiongozi huyo ametangaza kwamba yeye ni mtume na amekuwa akisema kwamba kupitia huduma yake anaweza kuwaponya watu wenye magonjwa yasiyotibika katika hali ya kitabibu, kama vile HIV na UKIMWI
katika ibada iliyofanyika jumapili ya jana kanisani hapo, kulitangazwa kwamba kuna maji matakatifu ambayo yana nguvu na uwezo wa kuwabariki na kuwaponya watu magonjwa yao, kwahiyo katika msongamano huo wa kuwania kupata maji hayo kutoka kwa mtume Tb Joshua, ndipo wanne wakapoteza maisha na wengine 13 kujeruhiwa vibaya
Habari na ripoti kuhusiana na kanisa la Tb Joshua, zimekuwa zikileta utata miongoni mwa watu wengi kuhusiana na yale yanayotokea ndani ya kanisa la Scoan, wapo wanao amini na wapo wasio amini. kutokana na utata huo watu wengi wamekuwa wakienda kupata huduma, katika utafiti, idadi kubwa ya watu ni wale wanaotoka nje ya nchi na idadi ndogo ikiwa ni ile ya wakazi wa Nigeria, katika nchi mbalimbali, kumekuwepo na mawakala wa kanisa la Tb Joshua, ambao uwapangia watu zamu za kwenda huko kuombewa na kutayarisha taratibu za vibali vya kusafiria (visa)
hii ni changamoto kubwa kwa viongozi na watumishi wa Mungu, kwakuwa wanatakiwa kuwambia watu na hasa waumini wao, nini ukweli kuhusiana na maji haya yanayo tolewa kwa imani ya kuwaponya na kuwabariki watu, je maji haya yantajwa wapi katika vitabu vitakatifu kuwa yanaponya? na je maji haya yanpatikana wapi na je tunaweza kutumia hata ya hapa kwetu nayo yakaponya? au lazima yawe yametoka kwa mtume Tb Joshua?
ni mambo ambao yanatakiwa kutolewa ufafanuzi na viongozi wa kanisa kuhusiana na utata unaozidi kujitokeza na changamoto zilizopo, kwavile, bado kuna wale wanao amini juu ya uponyaji kwa Jina la Yesu na wengine kutumaina zaidi maji haya ya uponyaji
Jumapili, 19 Mei 2013
Call Us Now:
+255 655 732121,
+255 716 758595 / +255 762 758595