Maneno katika kitabu cha Biblia, yanasema kutoka katika sura ya Yakobo 4:14, Walakini hamjui yatakayo kuwako kesho, uzima wenu ni nini? maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha utoweka.
Pia watu wa waliowahi kuishi Duniani, katika hisia zao walisema na kutamka maneno kama ya Mwimbaji na msanii marehemu Remy Ongala, ya kwamba Kifo hakina huruma! ujumbe huo wa Remy ambao ulipendwa na watu wengi, kifo hakina huruma!, ni maneno yaliyowatoka wakazi wa mjini Musoma, mwaka jana wakati wa mazishi ya marehemu Flora Mhere, leo ametimiza mwaka mmoja tangu mauti ilipomkuta, kifo kilicho tokana na ajali mbaya ya gari katika kijiji cha makutano (ziro ziro) gari aliyokuwa amepanda marehemu Flora Mhere ilikuwa imesimama bembeni kabisa mwa barabara kuu ya Musoma kwenda Mwanza, gari jingine zaidi ya tani 7 lilipoteza mwelekeo na kwenda huko ilipokuwa imesimama gari ya Flora Mhere, gari alimokuwemo iligongwa vibaya na kumsababishia maumivu makali Flora Mhere, alikimbizwa hospitali ya mkoa wa Mara wakijaribu kuokoa maisha yake, lakini mnamo tarehe kama hii mwaka jana alifariki akiwa anatibiwa katika hospitali ya Taifa muhimbili
Ajali ilitokea mnamo tarehe 15-3-2012 majira ya saa sita mchana, familia
yake, yaani mama yake mzazi Thereza Mhere na ndugu zake, wanapenda
kutumia nafasi ya siku ya leo, kuwashukuru wale wote walioshirikiana nao
tangu siku ilipotokea ajali hadi siku ya mazishi, wengi mlitusaidia
sana katika maombi, faraja, michango na mengine mengi, tunawashukuru
sana wote kwa msaada wenu mkubwa, tunawashuru hata wale waliotusaidia katika eneo la matibabu, madaktari na wauguzi wa hospitali ya mkoa wa mara, hospitali ya Bugando Mwanza, hospitali ya Taifa Muhimbili, Mungu awabariki kwa kila chema mlichofanya kwaajili yetu, tunathamini sana mchango wenu na ushirikiano wenu mkubwa mlioonyesha wakati wa kuuguza hadi wakati wa kifo.
Ijumaa, 17 Mei 2013
Call Us Now:
+255 655 732121,
+255 716 758595 / +255 762 758595