Mlinzi
wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya
Morogoro Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni mkoani hapa Bw
Mika Athumani amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.Habari
zilizoptaikana eneo la tukio zilidai kwamba majambazi hao baada ya
kuvamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane na kumvamia mlinzi huyo
na kumchinka kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuimba vitu mbali
mbali.
Umati wa watu ukishuhudia tukio hilo muda mfupi uliopita, haya ndugu, wanadamu tunafikia hatua ya kuchinjana kama kuku, hii inauma sana
Baadhi
ya watu waliokuwepo eneo hilo la tukio walidai kwamba mlinzi huyo
alikuwa amelala hivyo majambazi hayo yalimvamia na kumpora siraha zake
na kishi kumchinja shingoni," siumeona alikuwa amelala jirani na
baiskeli yake ndio maana ameshindwa kupamabna nao hasa ukizingatia baa
hii imejitenga iko peke yake hapa jirani na mto wa Morogoro"alisema Bw
Maneo Mashani.
Mtandao
huu ulishuhudia mtoto wa marehemu pamoja na mjukuu wa marehemu
wakiangua vilio eneo la tuko baada ya kuuona mwili wa mzazi wao
aliyeuwawa kikatili baadae wote wawili walipanda gari la polisi na
kuondoka nao.