Rais Robert Gabriel Mubage ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa rais
nchini Zimbabwe unaobishaniwa, matokeo rasmi yameonesha jana
Jumamosi(03.08.2013), wakati wapinzani wameapa kupinga matokeo.
Marekani wakati huo huo imesema kuwa uchaguzi huo si wa kuaminika.Mugabe mwenye umri wa miaka 89, ameonekana kurefusha utawala wake wa miaka 33 kwa kipindi kingine cha saba akiwa madarakani baada ya kumshinda kwa kishindo hasimu wake wa muda mrefu wa kisiasa , Morgan Tsavangirai , katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatano.
Matokeo rasmi yanaonesha kuwa Mugabe ameshinda kwa asilimia 61 ya kura za urais na wingi mkubwa katika bunge, akimgaragaza Tsvangirai ambaye ameambulia asilimia 3
Ashutumu uchaguzi
Lakini Tsvangirai mwenye umri wa miaka 61, ambaye bila mafanikio amekuwa akijaribu kumuondoa madarakani Mugabe kwa mara tatu, ameshutumu uchaguzi huo kuwa umeendewa kinyume na ni wa udanganyifu.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry wakati huo huo ametoa taarifa jana Jumamosi(03.08.2013) akiueleza uchaguzi huo kuwa " unamapungufu mengi".
"Marekani haiamini kuwa matokeo yaliyotangazwa leo wanawakilisha mtazamo wa kuaminika wa mapenzi ya watu wa Zimbabwe," Kerry amesema.
Tsvangirai ameapa kupambana na matokeo hayo mahakamani na kusema chama chake cha Movement for Democratic Change , MDC kitasusia taasisi za serikali.
"Hatutajiunga na serikali," Ames
Ametetea uamuzi wa MDC wa kuingia katika serikali ya kugawana madaraka na Mugabe, ambaye alitoa amri ya kukamatwa kwake, kupigwa na kfikishwa mahakamani kwa madai ya uhaini.
"Kushiriki kwetu kumeiokoa nchi hii. Shule zilifungwa, hospitali zilifungwa. Tulikuwa tunatumia sarafu ya Zimbabwe dolla ambayo haikuwa na thamani, hakukuwa na bidhaa katika maduka, kila mtu alikuwa katika mtafaruku," amesema.
Lakini akiwa amekasirika kutokana na kiwango cha udanganyifu katika uchaguzi mara hii, Tsvangirai amesema siku ya kuishi na mambo hayo zimekwisha.
Chama cha MDC sasa kina hadi Jumatano ijayo kuwasilisha ushahidi wake wa udanganyifu katika mahakama kuu, lakini kutafuta ushahidi mzito huenda litakuwa jambo gumu.
Tsvangirai amesema kuwa atawasilisha waraka wa "mapungufu yote na hali zote za kuendewa kinyume na sheria" kwa jumuiya ya kiuchumi ya kusini mwa Afrika SADC na kutoa wito wa kuitishwa kikao cha dharura cha jumuiya hiyo.
Kerry amesema kumekuwa na mapungufu katika utengenezaji wa daftari la wapiga kura , na kuongeza kuwa "Vyama havikuwa na nafasi sawa katika vyombo vya habari vya dola. Sekta ya usalama haikulinda hatua za kuelekea katika uchaguzi katika kiwango sawa."
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague ameeleza "wasi wasi wake mkubwa" kuhusiana na uchaguzi ulivyoendeshwa katika koloni hilo la zamani la Uingereza.
Jumuiya ya kimataifa ina wasi wasi
Umoja wa Ulaya , ambao ulikuwa unaelekea katika kulegeza vikwazo vya muda mrefu, umeeleza wasi wasi wake juu ya "kutokamilika kwa ushiriki wa wapiga kura, pamoja na kuelezea udhaifu katika hatua za mchakato wa upigaji kura pamoja na ukosefu wa uwazi."
ema. "Tutakwenda mahakamani."
Zimbabwe yatumbukia katika mkwamo
"Udanganyifu na kuiba kura katika uchaguzi huo kumeiingiza Zimbabwe katika mzozo wa kikatiba, kisiasa na kiuchumi."
Lakini Emmerson Munangagwa, waziri wa ulinzi na mshirika mkuu wa Mugabe, amejibu shutuma hizo na kudai kuwa matokeo hayo ni mabadiliko ya mchezo.
"Mataifa ya magharibi sasa yatabidi kushuka , yanapaswa kufatuta ngazi na kushuka ... uchaguzi wa kidemokrasia umefanyika nchini Zimbabwe," ameliambia shirika la habari la AFP.
Majirani wa Zimbabwe wameuidhinisha uchaguzi huo kwa kiwango cha juu.
0 comments:
Chapisha Maoni