Na John Nditi,
Morogoro.
KATIBU wa Jumuiya ya Kiislamu
nchini , Shekhe Ponda Issa Ponda, alijikuta katika wakati mgumu baada ya
kuumizwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni risasi kwenye bega lake la kulia wakati
akiekelea katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja wa Mjini Morogoro baada ya
kumalizika kwa kongamano ya Dini ya Kiislamu.
Mkasa huyo ulitokea Jumamosi Augosti
10, mwaka huu majira ya saa 12: 15 za jioni eneo la barabara ya Tumbaku karibu
na Fire, mara baada ya kumaliza kwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye
uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba , Manispaa ya
Morogoro.
Shekhe Ponda alishiriki katika
Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu Mkoani
Morogoro na kufanyika siku ya Idd Pili kuanza saa nane mchana hadi kumi na
mbili jioni ya siku hiyo.
Kongamano hilo lilipata baraka
zote na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, ambalo lilitoa masharti kadhaa
ya kuzingatiwa na wazungumzaji ikiwa ni kutokashifu dini nyingine wala viongozi
wa serikali.
Sakata la kutaka kutiwa mbaroni
kwa Shekhe Ponda lilikuja baada ya yeye kudaiwa kukiuka masharti ya Mahakama
aliyopewa baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje wa kutakiwa
asitende kosa lolote la jinai anapotumikia adhabu hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi
ya Kongamano hilo, Ustaadhi Idd Msema, alidai kuwa Shekhe Ponda baada ya kutoka
ndani ya gari eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege aliofika mita
chache katika barabara ya Tumbaku alitelemka na wakat akitaka kuingia garini
ilifayuliwa risasi iliyompiga begani.
Ustaadh Msema alidai kuwa baada
ya kupigwa risasi begani waumini waliokuwa wameambatana naye walimchukua na
kumpakiza kwenye Piki Piki hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili
kupoatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo,
baada ya kufika hospitali, waliona anacheleweshwa kpatiwa matibabu na ndipo
walipoamua kumwondoa na kumpekea kwenye Hospitali binafsi ambayo hakupenda
kuitaja.
Akizungumzia kwa kina hali ya Shekhe
Ponda baada ya kujeruhiwa huko, alisema kuwa yu hai licha ya kuumia vibaya
begani na kwamba wanatarajia kumpekela eneo jingine hususani Jijini Dar es
Salaam kupata matibabu zaidi.
Alisema viongozi wa Umoja huo hauwezi
kuweka wazi sehemu anakotibiwa kwa kuwa jambo hilo ni la kiusalama zaidi hasa
wakati huu ambapo kumekuwa na sinto fahamu.
Baadhi ya walinzi wa Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Morogoro waliozungumza juu ya tukio hilo , walikiri kuwa Shekhe
Ponda aliletwa hapo kwa usafiri wa Piki piki zikiambatana na nyingine zaidi ya
50 na kuishia getini.
Walisema walimwingiza adi
mapokezi na kwamba walipoona umati mkubwa upo getini waliamua kutoa taarifa
Polisi kuwa wamevamiwa na watu ambapo muda si mrefu Polisi wa FFU waliwasili na
gari lao Hospitalini hapo.
Hata hivyo walinzi hao walisema,
baada ya kuona Askari wamefika Hospitalini hapo, baadhi ya wafuasi wa Shekhe
Ponda waliamua kumyanyua na kumbeba mabegani na kutoka naye mlango mwingine
wakimlazimisha mlinzi kuwafungulia mlango na baadaye wakatokomea naye kwa
usafiri wa Pikipiki kusikojulikana.
Kufikishwa kwa Sheshe Ponda katika
Hosipitali ya Rufaa kulithibishiwa pia na Mwenyekiti huyo ambaye alidai
kuwa waliamua kumwondoa baada ya kuchekewa kupatiwa huduma.
Baada ya tukio hilo, uvumi ulisambaa
meneo mbalimbali nchini ukidai kuwa Shekhe Ponda amepigwa risasi na Polisi na
kufariki dunia. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Feustine Shilongine
akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi majira ya saa tatu usiku wa Augosti 10,
baada ya kutokea kwa tukio hilo, alisema kuwa hapakuwa na taarifa juu ya
kutokea kifo cha Shekhe Ponda.
“ Nimepingiwa simu zaidi ya 50 ,
zikiulizia jambo hili...kuwa Ponda amefariki dunia ...Binafasi nami ninazisikia
, ujumbe umesambazwa kwenye simu za watu mbalimbali...tumezunguka kila mahali
hakuna kifo wala maiti yake ...na vijana wangu wanaendelea kulifuatilia suala
hili” alisema Kamanda huyo.
Juhudi za kufuatilia sakata la uvumi
kifo cha Shekhe Ponda uliendelea kufanyiwa kazi na Ripota a wetu huyu na usiku
wa saaa tano Mwenyekiti wa Kamati huyo aliweka wazi kwa kusema kuwa Shekhe
Ponda yu hai isipokuwa ameumia vibaya sehemu ya bega .
“ Nipo katika eneo ambalo Shekhe
Ponda anapatiwa matibabu...sehemu ambayo hatuwezi kupataja kiusalama , isipo
kuwa ameumia vibaya kwenye bega lake. Lakini yu hai wala hajafa” alisema Msema.
Polisi Mkoani hapa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na sakata hilo, nasi
twaendelea kufuatulia kwa ukaribu
0 comments:
Chapisha Maoni