Jumamosi, 4 Mei 2013
Kwa kawaida maoni ya mtu utolewa baada ya mtoa hoja kuzungumza, lakini leo sauti ya kanisa inaomba kutoa mtazamo au maoni yake juu ya jukwaa la wakristo na majukwaa mengine kama yapo, nadhani yapo pia ya wahindu, waislamu, wapagani na wale wanaotambika kule milimani nk, kwa vile nafasi ni chache leo naomba nizungumze na kutoa mawazo yangu kuhusu kauli ya kumtaka Rais afanye kitu furani, tunataka Rais atoe tamko, tunamtaka Rais azungumze au aeleze jambo furani.
Nadhani kauli hiyo ni nzito sana na pia kwa mtazamo wa Biblia naona inakingana kwa sehemu kubwa, nafasi ya Rais au mkuu wa nchi inatajwa katika Biblia, na pia wajibu wa wakristo wote, wakiwemo jukwaa la wakristo, nafasi ya Rais wa nchi inatajwa ni MWENYE MAMLAKA, yaani mwenye kauli na tamko la mwisho, na nafasi ya wakristo ni UTII KWA MWENYE MAMLAKA, naomba niseme hivi, kauli zetu na hasa watu wa imani ni muhimu zilingane na imani yetu, kinyume cha hapo tutakuwa hatutendi haki na pia tunaikosea imani yetu, Rais kauli yake ni kwamba wakristo na waislamu waishi kwa amani, ndiyo aliyotoa majuzi pale Mbeya kwenye sherehe za mei mosi, hiyo ndiyo KAULI NA TAMKO LAKE, wewe unataka kauli natamko gani lingine? kuna siku nilikuwa natazama altare au madhabahu ya Askofu Kakobe pale mwenge, imeandikwa hivi, TAFUTENI KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE Waebrania 12:14, nadhani huu ndio unapaswa kuwa msingi wa ndugu zangu wakristo kuhusu suala la amani, jukwaa la wakristo na wakristo mnatakiwa kutafuta amani na watu wote, sio kusubiri kwa kumtaka JK kutoa tamko!! baba Askofu Ngalalekumtwa na wengine wote kwa majina ya uchungaji mitume wainjilisti manabii mapadre nk, imani yetu ni kubwa kwenu pale mtakapo nena yaliyosawa`na kweli ya Injili
wiki ijayo nitazungumza juu ya habari za kuchicha, lakini kwasasa nikuache uendelee na kauli ya jukwaa la wakristo
Jukwaa wa Wakristo Tanzania limemtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa msimamo wake kisheria ambao utaleta upatanisho kati ya waumini wa dini ya Kiislamu na Kikristo.
Jukwaa hilo limesema kauli iliyotolewa na rais
juzi wakati wa sherehe za Mei Mosi, Mbeya ya kutaka Watanzania waishi
kama zamani ina utata kwa sababu imetafsiriwa tofauti na baadhi ya
Watanzania.
Hivi karibuni Rais Kikwete wakati akizungumza
kwenye sherehe za Mei Mosi alisema Serikali bado inaendelea kuzungumza
na viongozi wa dini wa pande zote na kuwaunganisha ili kuona maelewano
yanarejea kama ilivyokuwa zamani na kuwataka Watanzania waendelee kuishi
bila kubaguana au kuchukiana kwa dini zao.
Akizungumza jana, Mwenyekiti wa jukwaa hilo,
Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu
wa Kikatoli Tanzania (TEC), alisema licha ya maneno hayo kuwa mazuri
lakini bado kuna utata kwa sababu baadhi ya raia wameingiwa na wasiwasi.
Alisema maeneo mengine wakristo hawali nyama kwa
sababu hawataki kulazimishwa kula nyama zilizochinjwa kwa ibada za
kiislamu na kwamba suala hilo siyo dogo kama wengine wanavyofikiri kwa
sababu limegharimu maisha ya watu.
Alisema licha ya kuwapo kwa kauli za uchochezi wa
kuwaua viongozi wa dini ya kikristo,kuchoma makanisa na mauaji ya
viongozi wa kikristo bado hazijafutwa wala waliozitoa hawajakamatwa na
kwamba hawajui kinachoendelea.
Mwenyekiti huyo alisema madai ya msingi ya
waislamu yaliyosababisha waanzishe vurugu na mauaji hayajajibiwa na
Serikali huku maswali yaliyoulizwa na wakristo kutokana na madai hayo na
vurugu hizo nayo yakiwa hajayajibiwa.
Alisema licha ya kukutana na Rais Kikwete Aprili
23, mwaka huu ambaye alihimiza viongozi wa wakristo na waislamu wakutane
ili kuondoa tofauti zao zisizo za kiimani lakini bado wanasubiri
maelekezo toka serikalini kwani ajenda ya uvunjifu wa amani viongozi wa
dini hawawezi kuizungumzia kwa sasa bila majibu ya Serikali kwa madai
yaliyozua uvunjifu huo wa amani.
0 comments:
Chapisha Maoni