Jumapili, 5 Mei 2013

TUKIO LA KUSHITUA KATIKA IBADA ARUSHA; KANISA LASHAMBULIWA KWA BOMU!!!

Mripuko kanisani Arusha wauwa mmoja

katika hali isitegemewa na Watanzania wengi, leo jijini Arusha limetokea shambulio la bomu ndani ya jengo la ibada katika kanisa la Katoliki Olasit nje kidogo ya mji wa Arusha, nani kafanya hivi? kwasababu gani? ili iwe nini? ni maswali ambayo yanaendelea kuumiza vichwa vya Watanzania wengi kwakuwa majibu ya maswali hayo ni magumu kutokana na amani iliyozoeleka katika nchi yetu

Takriban watu zaidi ya 46 wamejeruhiwa na mmoja kufariki katika tukio la bomu lililotokea ndani ya kanisa katoliki nje kidogo ya mji wa Arusha kwenye mripuko wa bomu kama saa tano asubuhi katika kanisa katoliki la Olasit nje kidogo ya jiji la Arusha!!! 


Wengine kadhaa walijeruhiwa huku balozi wa papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya kuzindua parokia mpya ya mtakatifu Yosefu walinusurika.
Kwa mujibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni paroko msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Arusha, mripuko ulipotokea walikuwa tayari kubariki maji kwa ajili ya uzinduzi wa kanisa, shughuli iliyokuwa ikiongozwa na balozi wa Papa Francis.
Hata hivyo Padre Mangwangi amesema kuwa taarifa walizonazo muda mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali, kuna mtu mmoja amefariki na wengine wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru mjini Arusha

Watalaalamu wa miripuko na polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo.
Bado hakuna taarifa ya chanzo cha mripuko au kama kuna mtu au kundi lilohusika.
Hili ni shambaulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japokuwa mwaka huu pia kulikuwa na tukio la mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani Zanzibar, ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia kanisani.


Sauti ya kanisa imefanikiwa kupata baadhi ya majina ya walio jeruhiwa katika mlipuko huo:-

EDITHA NDOWO 2. CHRISTOPHER RAYMOND 3. FRANK DONATUS 4.ELIZABERT ISIDORI 5. NEEMA DAUDI 6.AGRIPINA ALEX 7. ANOLD ALEX 8. SOPHIA KOMOLA 
9.LOVENESS NELSON 10. THEOPIDA INOCENT 11. FAUSTINE ANDREA 12. REGINA DANIEL 13. JOYCE YOHANA 14. GENERS PIUS 15. MASWEET SERIRI 16. JAMES GAMBRLE 17. ANOLD SWAI

Haya ni baadhi ya majina, majina mengine sauti yakanisa itakuletea wakati wowote baada ya kuyapata majina hayo kutoka kanisani katoliki au popote pale kilipo chanzo chetu cha habari
 Ndugu zangu kitendo cha kuua ni tendo linalo mchukiza sana Mungu, na ndio sababu alisema kati ya moja ya amri zake USIUE!! na kila atakayeua itampasa kutupwa katika moto yaani kwenye mateso milele, kaini alipomuua ndugu yake Mungu akichukizwa sana na lile jambo, akampa adhabu kubwa kaini, tunaliomba Jeshi la polisi na idara zote zinazo husika wachukue hatua kwa kila atakaye bainika kwa kuhusika na tukio ili baya, Pia sauti ya kanisa inachukua nafasi hii kuwapa pole wakristo wote waliokuwa katika ibada hiyo, poleni kwa yote yaliyo wapata, Roho Mtakatifu awape faraja na kuwaponya majeraha yote mliyopata, na wale waliokufa, neno linasema HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA, ikiwa mmekufa katika Bwana mna heri nyingi

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA NA MAELEZO YA MKUU WA POLISI MKOA WA ARUSHA. MWANAKWAYA 1 AFARIKI

  Hali ya eneo mlipuko ulipotokea

Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea

Ulinzi umeimarishwa

Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Wanausalama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio

Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi. 
 
Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.

JAMANI JAMANI JAMANI KWANINI HAYA YATOKEE!!! Tuingii katika maombi kwaajili ya Taifa ili amani ipatikane na upendo wa Yesu uonekane na kutawala. poleni nyote mlipatwa na matatizo haya pamoja na kufiwa na ndugu zenu, msiba huu ni wetu sote wapenda amani na watanzania wote

 

0 comments:

Chapisha Maoni

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595