Ni kweli na hakika Neno la Mungu linasema mshahara wa dhambi ni mauti!! kwanini utafute pesa au mafanikio kwa njia ambayo sio halali? kwanini usitumie njia halali na nzuri ili hata baada ya kufanikiwa uwe na amani na yale mafanikio uliyoyapata? hawa ndugu zetu walikwenda kutafuta pesa na mafanikio kwa njia ambazo sio nzuri kwa jamii na hata mbele za Mungu, yaliyowapata ni mabaya sana!! wamekutana na polisi na hatimaye kupoteza maisha yao, na la kuumiza zaidi waliofikwa na hayo bado ni vijana, kiasi kwamba wangeweza kufanya kazi wakafanikiwa, wanamaeneo mazuri ya mashamba, wangeyatumia leo wasingefikwa na yote haya! fuatana nami sasa uangalia tukio lililotoke kwa kutazama habari picha
|
Baadhi ya wananchi wakitoka kutambua miili ya wanaodhaniwa kuwa ni majambazi |
|
Tunaomba radhi kwa kuonyesha picha hizi kwani mpaka sasa maiti hizi hazijatambulika |
|
Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika siraha |
|
Hii ndiyo Gari iliyotumiwa na majambazi hayo |
|
Siraha walizokuwa wanatumia majambazi hayo |
|
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa
Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana
katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya
Tukuyu.
|
Mtandao wa majambazi, unazidi
kusambalatishwa nchini, hasa katika mkoa wa Mbeya, hii ni baada ya kuuwawa watu
watano wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika mashambulizi ya majibizano kati ya
hao waliouwawa na askali wa jeshi la polisi mkoani Mbeya. Kamanda wa polisi
mkoani Mbeya amewaambia waandishi wa habari alipokuwa akizungumza nao ofisini
kwake kuwa, tukio ilo limetokea majira ya saa sita mchana katika kijiji cha
Garijembe mkoani Mbeya kwenye barabara ya Mbeya Tukuyu. Kamanda wa mkoa Diwani
Athumani, alisema jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa kitengo chake cha
upelelezi, ndipo wakaweka mitendo ilifanikisha kuwanasa majambazi hao wakiwa
ndani ya gari yao yenye namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota spacio.
Askali walipoiona gari hiyo
waliyokuwa wanaishuku, ndipo walipochukua hatua ya kuisimamisha gari hiyo,
matokeo yake, wale majambazi walianza kurusha risasi ovyo ovyo kujaribu
kuwazuia na kuwashambulia askali wa jeshi la polisi, ndipo askali nao
walipoanza kujibu mapigano hayo, na matokeo ni kwamba, majambazi wote
walijeruhiwa na wakakamatwa na kukimbizwa katika hospitari ya rufaa mbeya,
kufika hospitali, daktari akithibitisha kuwa tayari wamekwisha kufa.
Kamanda Diwani Athumani aliongeza
kwa kusema kuwa, baada ya upekuzi uliofanyika, walibaini bunduki mbili, moja ni
smg yenye namba 848628 iliyobaki na risasi 16 baada ya risasi nyingine kutumika
na majambazi hao katika majibizano na polisi, na nyingine ni Mark III yenye
namba iliyokuwa na risasi mbili na koa la shaba
Kamanda Diwani Athumani aliongeza
na kusema, majina ya majambazi hao hayakuweza kufahamika mpaka wakati anaongea
na wanahabari, lakini akatoa wito kwa wananchi kwenda katika hospitali ya mkoa
wa Mbeya kwa lengo la kutambua miili ya marehemu hao, ili wakabidhiwe kwaajili
ya taratibu za mazishi, kamanda akamalizia kwa kuwaomba wananchi kutoa taarifa
za mienendo ya watu isiyo ya kawaida au wanaotiliwa mashaka, toeni taarifa
katika mamlaka husika na kwa wakati.
Sauti ya kanisa, imesikitiswa na tukio ilo, kwa
kuwa wote waliouwawa ni vijana na walikuwa na uwezo wa kufanya kazi halali na
kupata mahitaji yao muhimu, lakini ikumbukwe pia kwamba, hao walio kufa,
kuna usemi usemao, wametangulia mbele ya haki, je ni haki ipi wataipata mbele
za Mwenyezi Mungu ikiwa mauti imewakuta katika tukio la wizi? Jibu nakuachia
mwenyewe mpendwa msomaji.
0 comments:
Chapisha Maoni