Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tukio la Mwanafunzi kukatwa Koromeo. |
MWANAFUNZI
wa Darasa la kwanza katika shule ya msingi kijiji cha Tatu kata ya
Kiomboi tarafa ya Kisiriri wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida,Geofrey
Emmanuel (9) amefariki dunia baada ya kukatwa koromeo kwa kisu na
kusababisha kuvunja damu nyingi.
Inadaiwa
kuwa mwanafunzi huyo alichinjwa kinyama na Francis Lukumbitio (30)
mkazi wa kijiji cha Kizenga ambaye naye aliuawa na wananchi wenye hasira
kali kwa kumwagiwa Petroli na kisha kuwashwa moto.
Kamanda
wa Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo la
kusikitisha limetokea Desemba 15 mwaka huu saa 10.00 jioni katika kijiji
cha Tatu kata ya Kiomboi wilaya ya Iramba.
Amesema
siku ya tukio mwanafunzi huyo akiwa anachunga mbuzi pamoja na watoto
wenzake ghafla alitokea Francis akiwa amebeba kisu mkononi na kumshika
kwa nguvu na kuanza kumkokota hadi kichakani na kisha kutekeleza unyama
wake huo.
Akifafanua
zaidi, amesema wenzake waliweza kufuatilia na walipofika eneo la tukio
walikuta mwanafunzi huyo tayari amekwishafariki dunia kutokana na
kukatwa koromeo.
“Watoto
hao baada ya kuona tukio hilo, walitoa taarifa kijijini na haraka
wananchi waliweza kukusanyika na kumfuata mtuhumiwa kijijini kwake
Kizega na walifanikiwa kumkuta Francis akiwa nuyumbani kwake Walimtoa
nje na kuanza kumpiga kwa fimbo, marungu na mawe na alipokuwa taabani
walimwagia petroli na kumwasha moto”,amesema Kamwela.
Kamanda
Kamwela amesema wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na mauaji hayo
ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuacha mara moja tabia ya
kujichukulia sheria mkononi na badala yake wawafikishe watuhumiwa kwenye
vyombo vya dola ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni