Makubaliano ya uwekezaji huo mkubwa yameshuhudiwa leo (Alhamisi, Oktoba 24, 2013) na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mawaziri wengine wa Serikali baada ya
kusainiwa kwa mikataba saba ya uwekezaji katika sekta hizo muhimu kwa
uchumi wa nchi.
Utiaji
saini huo ulifanywa mara baada ya Waziri Mkuu kufungua Kongamano la
Uwekezaji na Biashara kati ya Tanzania na China (Tanzania China Business
Forum) uliofanyika kwenye hoteli ya Dong Fang, jijini Guangzhou jimboni
Guangdong, China. Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano
kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Baraza la Biashara la
China Afrika (China Africa Business Council-CABC) linashirikisha
wafanyabiashara wa China na Tanzania.
Mikataba
iliyosainiwa leo ni kati ya Shirika la Umeme (Tanesco) na Kampuni ya
Tabiau Electric Apparatus Stock Co Ltd (TBEA) ambao ni kwa ajili ya
ujenzi wa njia ya umeme ya msongo mkubwa wa 400kV katika Gridi ya Taifa
inayotoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini Mashariki hadi Arusha.
Kaimu
Mkurugenzi wa TANESCO, Bw. Felchesmi Mramba ndiye aliyesaini mkataba
huo wenye thamani ya dola za marekani milioni 692.7. Bw. Mramba pia
alisaini mkataba mwingine na kampuni ya Shanghai Electric Power ambayo
ndio itajenga mtambo wa Kinyerezi III.
Mkataba
mwingine uliotiwa saini na Mramba ni kati ya Tanesco na kampuni ya
China Gezhouba Group Corporation (CGGC) ambao wamekubali kuendeleza
mradi wa umeme unaotokana na nguvu ya maji wa Rumakali ambao uko katika
mikoa ya nyanda za juu kusini. Miradi hiyo miwili bado iko kwenye ngazi
ya upembuzi yakinifu hivyo gharama zake bado hazijajulikana.
Kampuni
ya Mkonge Energy Systems Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara wa
Tanzania, Bw. Salum Shamte ilitiliana saini mkataba na kampuni ya Sino
Hyro Resources Ltd kwa ajili ya kuendeleza umeme wa nguvu za maji wa
Masigira. Mradi huo unagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 136.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bw. Nehemia
Mchechu aliweka saini mkataba baina ya NHC na kampuni ya China Railway
Jianchang Engineering (CRJE) kwa ajili ya kuliwezesha kifedha shirika
hilo liweze kujenga nyumba mbalimbali za makazi na biashara nchini.
Mradi huo una thamani ya dola za Marekani milioni 500.
Bw.
Mchechu pia aliwekeana saini mkataba mwingine na kampuni ya Poly
Technologies (POLY) wa kuwa na uhusiano kifedha na kiufundi kati ya
kampuni hizo ya kichina na NHC kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi na
biashara huko Masaki wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Gharama
za mradi huo ni dola za Marekani milioni 200.
Mkurugenzi
wa Shirika la Maendeleo (NDC) Bw. Gideon Nassari kwa niaba ya shirika
lake aliingia mkataba na kampuni ya China ya Dalian International
Economic & Technical Gooperation Group (CDIG) na Kampuni ya Hydro
China Kunming Engineering Corporation kwa ajili ya kujenga kituo cha
utafiti na mafunzo ya nishati mbadala. Mradi huo una thamani ya dola za
Marekani milioni 136.
Mramba
na Mchechu kwa nyakati tofauti walisema kwamba utekelezaji wa miradi
hiyo utaanza wakati wowote kwani mambo mengi walishayakamilisha kwenye
mazungumzo.
Wakati
utambulisho, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bibi Julieth Kairuki alisema
jumla ya Makampuni na Taasisi 46 zinazowekeza na kufanya biashara
Tanzania zinashiriki katika Kongamano hilo ambapo kwa upande wa China,
CABC wameandikisha makampuni 44 yatakayoshiriki kwenye kongamano. Katika
Kongamano hilo, TIC imewasilisha mada ya mazingira ya uwekezaji
Tanzania na Bodi ya Utalii na Shirika la nyumba la Taifa wamewasilisha
mada zinazohusu uwekezaji kwenye sekta ya Nyumba na fursa za utalii
nchini Tanzania
Waziri
Mkuu ambaye yuko katika siku ya nane ya ziara yake ya kikazi kwa
mwaliko wa Serikali ya China bado anaendelea na mikutano mbalimbali na
leo usiku atazungumza na Watanzania waishio Guangzhou
0 comments:
Chapisha Maoni