Mkuu
wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji(NIT) Dk.Zacharia Mganilwa
(kushoto) akimkabidhi tuzo Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison
Mwakyembe(kulia) kwa mchango wake mkubwa wa kuboresha sekta ya
reli nchini kwa niaba ya kampuni ya Mwandi Tanzania kwenye hafla ya
makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Lorietha
Laurence
…………………………….
SERIKALI
inapata mapato ya takribani Sh. milioni 3.5 kwa siku sawa na zaidi
shilingi Bilioni moja kwa mwezi kutokana na usafiri wa treni katika
jiji la Dares Salaam.
Hayo yamesemwa
na Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji(NIT) Dk.Zacharia Mganilwa
wakati akimkabidhi tuzo Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe kwa
mchango wake mkubwa wa kuboresha sekta ya reli nchini kwa niaba ya
kampuni ya Mwandi Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika
leo jijini Dar es Salaam.
Aidha
Dk. Mganilwa tuzo pia imetolewa kutokana na Waziri Mwakyembe ameweza
kufufua na kuweka kwenye fikra Reli ya Musoma ya kwenda Arusha na Reli
Tanga.
Akizungumza
katika makadhiano hayo,Dk.Mganilwa amesema kuwa tuzo hiyo ilizingatia
vigezo vyote muhimu vya kumpata mshindi kwa kuzingatia mchango wa
muhusika katika sekta ya hiyo ,mtazamo wa wananchi kwa mtu husika na
msimamo binafsi wa mtu husika kwenye uboreshaji huo.
“Ninyi
ni mashuhuda wa mapinduzi ya usafiri wa treni za abiria jijini Dar es
Salaam unaowanufaisha zaidi ya abiria 14,000 kila siku na ikumbukwe
kwamba wazo la kuanzishwa usafiri huo lilikuwepo lakini Mheshimiwa
Waziri ndiye aliyekuja kufanya ndoto hiyo kuwa uhalisia”alisema
Dkt.Mganilwa.
Tuzo
hiyo imepatikana baada ya kushindanishwa kwa majina matatu ya watu
ambao wana mchango mkubwa kwenye maendeleo na mapinduzi ya reli Tanzania
kwa kurejea kila mmoja katika kipindi chake cha na kile alichokifanya.
Aidha
ameiomba Serikali kupitia wizara ya hiyo kuanzisha mfuko wa miundo
mbinu kwa fedha zitakazo kuwa zinapatikana katika usafirshaji ili kuweza
kuendelea kuboresha suala hilo na kukuza uchumi wa nchi yetu pamoja na
kuleta maendeleo.
Naye
Waziri Mwakyembe ameishukuru kampuni hiyo kwa kuuona mchango wake
katika jamii na kuweza kumpatia tuzo, ambayo ni motisha itakayo
muongezea juhudi za kuliletea Taifa letu maendeleo kupitia sekta ya
hiyo.
“Kwa
niaba ya TRL, RHACO na wafanyakazi wote wa wizara ya Uchukuzi napenda
kuishukuru kampuni ya Mwandi Tanzania kwa kuuona mchango wangu katika
sekta ya usafiri wa treni bado tunaendelea kuweka mipango madhubuti
kuboresha usafiri wa treni nchini na Afrika Mashariki kiujumla”alisema
Dkt.Mwakyembe.
Watu wengine
walioshiriki katika ushindani wa tuzo hiyo, Injia Festo Mwanyika na
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Reli Tanzania na Linford Mboma
kutoka Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA).
0 comments:
Chapisha Maoni