huyu ndiye aliyekuwa anaendesha pikipiki hiyo, hapa yupo katikati ya barabara akiwa amelala pasipo kujitambua na damu nyingi zikimtoka kichwani na maeneo mengine, yupo katika hali mbaya sana kiafya
huyu ni abiria aliyekuwa amepanda pikipiki hiyo hapo juu, anaangaika kwa maumivu makali aliyoyapata kichwani na mikononi, wote wawali walikuwa hawajavaa kofia za kujikinga na madhara ya kichwa.
huyu ndiye dereva wa gari iliyogongana na pikipiki hiyo bwana Fahad akipiga simu kuwajulisha ndugu na jamaa juu ya tukio lililo mpata, yupo ktk hofu kubwa kwakuwa hakutarajia yaliyotokea! muda mfupi baadhi ya ndugu zake walianza kufika katika eneo la tukio
katika hali ya mshangao wanatazama umati wa watu na mtu mmoja alilala, na hakuna anayeelewa kuwa huyu amekufa au la, mpaka hapo atakapo fikishwa hospitali Temeke kwa daktari kwakuwa yeye ndiye atakaye zungumza baada ya vipimo
tukio lingine lililotokea ni kwa askali polisi wa usalama barabarani, hapa ni wakati gari aina landrover ambalo ni maalum kwaajili ya kuvuta magari mabavu, limefika eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali, lakini linafika kwenye tukio na askali polisi, cha kwanza yule polisi anashughulikia lile gari kuvutwa na sio majeruhi kupelekwa hospitali, hapo ndipo wananchi wenye hasira walipotaka kumpa kipigo yule polisi na dereva wa ile gari, baada nzuri yule dereva akawa mpole akasikiliza walichotaka wananchi, kwamba awapeleka kwanza majeruhi hospitali na sio kuangalia pesa kwanza, kwa hakika ilikuwa patashika
hali ilikuwa mbaya sana, lakini hatimaye shari hiyo ilipungua baada ya wale majeruhi kupelekwa hospitali