Lakini wale wanamtegemea Mungu watakuwa
na mtazamo kwa Kimungu, na walio na
maisha ya jinsi hiyo, mtazamo wao uleta majibu ya mahitaji yao, kwa kuwa
matumaini yao yote wameweka kwa Mungu, hivyo watakuwa salama, Muinjilisti EVA
akasoma Neno kutoka katika kitabu cha Zaburi 145:18-20, akasema wanadamu
tukiweka tumaini letu kwake, Mungu uwa karibu yetu. Biblia inaposema Mungu
anakuita maana yake Mungu anakuita ili akubariki na kukuinua (Zaburi 34:2o),
alisema mtumishi huyo wa Mungu, kwahiyo wanaomtgemea Mungu watakuwa salama
maisha yao yote, Muinjilisti Eva akasema ikiwa tunapita katika mazito au mambo
mabaya yenye machungu, hii ni kwakuwa Mungu anataka yale mapito yetu
yauzindikize utukufu wa ushindi wetu unaokuja kwetu, waumini baada ya kusikia
hivyo walishangilia kwa makofi na vigelegele. Mungu alimchelewesha Sara kupata motto,
sababu ilikuwa ni kwamba Mungu alikuwa anaweka mashahidi wengi wa ushindi wa
Sara watao uthibisha utukufu wa Mungu kwa Sara!
Akasema, ndugu zangu tusiangalie
matatizo mengine ya watu na kuyafanya kama kanuni ya Mungu kwetu pia, eti
unasikia furani amekufa kwa ugonjwa kama huu wangu, nawewe ukasema utakufa,
hapana!, ndio sababu njia alizo pitia Elia, sio alizopitia Elisha. Na yale
aliyopitia Daudi siyo aliyopitia Sulemani, na ndio sababu Yakobo siku anashindana
na malaika ili ambariki, alipoulizwa jina lako ni nani, akasema yeye ni Yakobo,
na hakusema yeye ni mjukuu wa Ibrahim wa mtoto wa Isaka, kwakuwa aliamini yeye
ni tofauti na wote hao katika kanuni za majibu yatokayo kwa Mungu
Tatizo ulilonalo ni njia ya
kuleta ufumbuzi utakao kwa Mungu, ndio maana japokuwa Sara alikuwa tasa, lakini
Mungu alimtazama na kumwona ni mama wa mataifa mengi, mama wa uzao mkubwa sana,
Mungu ni huyo huyo, japo kuwa leo wewe ni tasa au unaukimwi au lolote, Mungu
anapokutazama anakuona wewe unao uzima tele, huu ni mwaka wako, aleluya, Zaburi
49:14-16
Hivyo ndivyo Neno la Mungu
lilivyokuwa Jumapili ya leo katika kanisa la Hopran linaloongozwa nan a Mchungaji
kiongozi JIMMY. Unakaribishwa katika ibada za wiki ijayo na jumapili