Alhamisi, 9 Mei 2013

TUTAWASAKA NA KUWAPATA WALIPUAJI - WAWE NDANI YA NYUMBA AU NDANI YA MAJI:- RAIS KIKWETE



"Waliofanya haya hawana pa kujificha, iwe ndani ya nyumba, nje ya nyumba, chini ya maji, ndani ya nchi, nje ya nchi - tutaendelea kuwatafuta mpaka tuwapate na kuwawajibisha." Ni kauli ya Rais Kikwete akizungumza na wananchiu kupitia wanahabari jijini Arusha siku ya Jumanne wakati alipotembelea jijni  kuwajulia hali majeruhi wa tukio hilo, akitoa salamu za pole na kuwahakikishia wananchi kuwa usalama utadumishwa na kuhakikisha kuwa wahusika wote wanakamatwa, kwani mpaka hivii sasa ulinzi kwenye mipaka yote ya karibu na tukio imeshaongezewa ulinzi na ukaguzi kufanyika kwa kila anayetoka.
Katika hotuba yake, Rais Kikwete amesena kuwa, "Watanzania waendelee kusali, wasiache kwa kuhofia kwa sababu ya watu fulani wenye roho mbaya, katili au watu waovu"  maana kwa kufanya hivyo watakuwa wametimiza azma ya washambuliaji hao, ya kutaka makanisa yawe matupu, bila waumini, na kusisitiza kuwa Serikali ipo na itaendelea kudumisha usalama.
"Tumeanza, hatutalala, tutakesha tutashinda, mpaka tuwakamate." Rais Jakaya Kikwete
Rais Kikwete pia amewataka wananchi kuepuka minong'ono ya mtaani na badala yake kutoa taarifa yoyote ambayo wanahisi itasaidia kukamata watuhumiwa zaidi kulekea kupata chanzo halisi cha mkasa huo.

"Tusiwasikilize wanaopotosha, kujitia mafundi walimuona fulani, alkuwa fulani, kama kuna mtu yeyote atoe taarifa pilisi, idara ya usalama wa taifa na hata kwa kiongozi yeyote kwa kuwa uchunguzi utafanyika"
"Hakuna taarifa yoyote ambayo tutaipata, hatutaifanyia kazi, kama ambavyo tumefanyia kazi hizi za mwanzo na tumewapata hawa tisa." Amesema Rais Kikwete.

katika hatua nyingine, kamati ya ulinzi na usalama ya bunge la Jmahuri ya Muungano wa tanzania imewasilisha hoja ya kufuta mihadhara yote ya kidini, ili kukabiliana na uchochezi na vurugu ambazo zinaweza kujitokeza. 

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595