Bahati Bukuku, wengi tunafahamu kutokana na kipawa chake cha uimbaji wa nyingi za Injili, amefanya kazi njema sana hapa Tanzania katika eneo la uimbaji, wengi wametiwa moyo nanyimbo zake, na hata wengine kuokolew pia, ameshilikiana na wahubiri wengi kufanya mikutano ya Injili nk. lakini kuna jambo ambalo tumelipata hivi punde kutoka katika gazeti mojwapo la linalotolewa siku kama hii kila wiki, habari zinasema kwamba alifanya mahojiano na mwandishi wa gazeti ilo, na kueleza kuwa kapata mchumba na anachosubiri ni kupewa taraka na yule mume wake wa kwanza, eti anasema, akiolewa na mume mpya kabla ya taraka, anaona atamkosea Mungu!! sauti ya kanisa inashangazwa na manene haya ya mtumishi wa Mungu Bukuku!! ni nani aliyemwambia Bukuku kuwa kuna taraka? bahati kwa mtazamo wangu angepaswa kujua kwamba, kwenye Ukristo taraka ipo na wala haipo mbali, ambayo Yesu ameipa jina kuwa ni KIFO, ndicho kitakacho watenganisha!! yeye anadai taraka mahakamani!! oooh ndugu zangu, tunapoona mambo kama haya, tujue ule mwisho unakaribia, tena pasipo aibu anakwenda kueleza nia hiyo ya kuolewa kwenye vyombo vya habari. naomba kusikia maoni yako ndugu msomaji wangu kuhusu habari hii ya bahati bukuku kudai taraka.
Haya sasa endelea kupata maneno ya bukuku mwenyewe hapa chini, haya ya mwanzo yalikuwa maoni yangu sauti ya kanisa
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI wa Muziki wa Injili mwenye muonekano wa ‘mama mwenye ndoa’, Bahati Lusako Bukuku amefunguka kuwa amepata mchumba lakini tatizo linabaki kuwa mume wake wa zamani, Daniel Basila ambaye anasuasua kumpa talaka yake, Amani lina mkoba mkononi.
Akizungumza na ‘balozi’ wetu jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia Haina Huruma aliweka ‘pleini’ kwamba hivi karibuni Mungu amemjalia kupata mchumba ambaye anahofia kumwanika kwa kuwa anabanwa na kifungo cha ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Basila.
Bahati alisema kuwa kifuatacho inabidi adai talaka yake kwa nguvu zote hata ikiwezekana kufikishana polisi ili aondokane na kifungo cha ndoa hiyo na aanze mipango ya ndoa kwa kuwa hataki kumtendea Mungu dhambi.
Alisema kuwa, mara nyingi amekuwa akimkumbusha mumewe huyo wa zamani kuhusu talaka lakini amekuwa akimwambia asikonde talaka yake ipo hivyo avute subira.
Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.

muta watambua kwa matendo , Mungu ni mwema kila siku
JibuFutamimi ni muinjisti ngoy stephene toka congo/bukavu