Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk
Emanuel Nchimbi akizungumza na wananchi katika viwanja vya mashujaa
Mnazi Mmoja muda mfupi baada ya kuweka shada la maua katika mnara wa
kumbukumbu ya mashujaa kuadhimisha siku ya walinda amani.
Tanzania
imeungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha siku ya walinda amani
katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo,pamoja na
kuwakumbuka walinda amani wapatao 3100 waliopeteza maisha wakati wa
kulinda amani.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho maadhimisho hayo alikuwa waziri wa mambo ya
ndani ya nchi Dk Emaanuel Nchimbi ambapo sherehe zilianza kwa gwaride na
kufutiwa na wimbo wa Taifa na baadaye wimbo wa Umoja wa Mataifa.
Dkt.
Nchimbi aliweka shada la maua katika mnara wa mashujaa akifuatiwa na
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mwakilishi wa Shirika la
chakula nchini Bwana Richard Ragan ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka
mashujaa ha o.
“Ni
muhimu kuikumbuka siku hii ambayo ilianzishwa na Umoja wa Mataifa wa
kulinda amani mwaka 1948 ambapo zaidi ya wanajeshi,polisi na wananchi
3100 walipoteza maisha katika harakati za kulinda amani, ” alisema
Dkt.Nchimbi.
Aliongeza
kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazojishughulisha na katika
sehemu mbalimbali zenye migogoro ambapo kwa sasa wanajeshi wapatao
1,300 wanaoshiriki kulinda amani nchini Sudan,Lebanoni, ,Ivory Coast
na Jamuhuri Kidemokrasia ya Kongo .
Akitoa
shukrani zake kwa jeshi la wananchi la kulinda amani , Jeshi la
Polisi na kituo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa kwa kuandaa tukio
hili Bw. Ragan ametaka watu wote waheshimu na kutambua wale wote
waliopoteza maisha wakati wa kulinda amani.
Siku
ya Maadhimisho ya Umoja wa Kimataifa ya kulinda amani ilianzishwa na
Umoja wa Mataifa mwaka 2002,kila mwezi Mei na imekuwa siku
maaluma kutoa heshima kwa wale walioshiriki katika kulinda amani.