Vipi ndugu yangu, uenda wewe ni mzazi au unandugu yako mwenye umri wa ujana, je ukimkuta anafanywa kama huyu hapa, utafanya nini, je utamtetea au utamsaidiaje? ungetamani kuwambia nini wale wanaompa kipingo? je utajitosha kumtetea? au utasema mpelekeni polisi?
wazazi tukae na watoto wetu kila wakati na kuwaonya wasitende maovu kama vile wizi, huyu naye pia amezaliwa na anao wazazi, sijui wakiona yanayo mpata mtoto wao inakuwaje moyoni mwao, uchungu!!
Tunaambiwa kuwa kuna maisha mengine baada ya kufa, je ndugu yetu kama huyu baada ya kifo hiki kinachotokana wizi anakwenda wapi! je amefanikiwa kuomba msamaha katika mateso haya?
Jamani ni vema kukumbuka kwamba hatupaswi kuua katika maisha yetu, Mungu anasema Usiue, hata kama tumefanyiwa jambo baya, hata kama mwizi katuibia, tusiue, mpeni nafasi ya kutubu, kuua ni jambo baya sana kwasababu ukimwaga damu ya mtu kwa kuua ile damu uliyoimwaga uwa inazungumza mengi na kulia sana juu ya yule anayefanya kitendo kile, inaweza kulipa kisasi na pengine kutamka laana!!
Jumatano, 29 Mei 2013
Call Us Now:
+255 655 732121,
+255 716 758595 / +255 762 758595