Jumatatu, 15 Aprili 2013

MAREHEMU MEJA JENERALI MAKAME RASHID AAGWA

Hatimaye marehemu meja jenerali Makame Rashid ameagwa rasmi kama ishara ya kusema kwamba hatutamwona tena, ndicho kilichofanyika jana kwenye kambi ya jeshi huko Mgurani Dar es salaam, na watu wengi walishiriki wakiwemo viongozi mbalimbali, na miongoni mwao ni Rais mstaafu awamu ya pili mzee Mwinyi, Rais mstaafu awamu ya tatu mzee Mkapa, makamu wa Rais, mkuu wa majeshi, mkuu wa jeshi la polisi, mkuu wa jeshi la magereza na wengine wengi

Karibia kila mtu aliyekuwepo alikuwa amefunikwa na majonzi makubwa, hasa ndugu wa karibu wa marehemu na wale waliofanya kazi na marehemu wakati wa uhai wake, wengi wanamkmbuka kwa upole na moyo wake wa huruma wa kujali na kupenda kuwasaidia wengine, ingawa alikuwa ni kiongozi mkubwa lakini bado alipenda na alijisikia amani kujichanganya na watu wa kila aina, umati mkubwa uliofurika unaonyosha jinsi alivyokuwa mtu wa watu.

kwa hakika ni kama wanavyosema wahenga, kazi ya Mwenyezi Mungu haina makosa, kikubwa kwako na kwangu na kwetu sote ni kutafakali juu ya mwisho wa maisha yetu utakuwaje, tukumbuke kwamba, mtu anapokufa si mwisho wa maisha yake, kuna maisha mengine baada ya kufa, na maisha hayo baada ya kufa yanategemeana na jinsi ulivyoishi hapa Duniani, kama ulitema mema kwa kuishi sawa na Neno la Mungu utakwenda kuishi na Mungu milele, na kama ulitenda mabaya utatupwa motoni alipo ibilisi na shetani!!
Rais mstaafu naye anatoa heshima zake mbele ya mwili wa marehemu Makame, alimjua na kufanya kazi naye enzi za uhai wake.
Je mwisho waetu sisi utakuwaje na utakuwa lini? hakuna anayejua siku wala saa, yaweza  kuwa leo, hatujui, kwa vile hatujui siku ya tukio kubwa kiasi hicho, ni vizuri kila wakati tuwe tumejihandaa, kwa njia ya kuishi maisha yaliyo safi yanayo mpendeza Mungu

Kifo limekuwa ni tukio lisilo zoeleka, unaweza kuzoea vitu vingine lakini sio kifo! japo nitukio la kila siku na ambalo tunalishuhudia mara nyingi, mwenyezi Mungu atusaidie sana katika maisha yetu haya mafupi hapa Duniani kumpendeza yeye, tunazaliwa, lakini baada ya kuzaliwa tunaishi kwa mud mfupi sana hapa duniani, na wakati mwingi uwa nasema hivi, je muda wangu uliobaki wa kuishi hapa Duniani ni miaka mingapi, hasa unapooanisha ni umri wa kawaida wa maisha ya uhai wa kiumbe mwanadamu, wanasema umri mkubwa ni miaka 70 au 80!! je katika hiyo tumebaki na miaka mingapi? ingawa tena tunaambiwa kifo hakichagui mzee au mtoto au kijana!! yaweza kuwa kwa sababu ya ajali, au homa au wengine wanakwenda kulala wakiwa wazima lakini kifo kinawakuta kwa kuuawa na majambazi nk!
MAKAMANDA WA JWTZ WAKIUWEKA MWILI SEHEMU MAALUMU KWAAJILI YA KUWAPA NAFASI WATU WOTE KUTOA HESHIMA ZA MWISHO
NDUGU WA MAREHEMU WAKIWA KATIKA MAJONZI MAKUBWA, KWA KUONDOKEWA NA KIPENZI CHAO JENERALI MAKAME RASHID.
MAREHEMU ALIKUWA NI MKUU WA JKT MSTAAFU, NATAMBUA MAKAMANDA HAWA NAO WALIMJUA VIZURI NA WALIFANYA KAZI NAYE KWA KUJENGA TAIFA, UENDA WANATAFAKALI MENGI WANAPO SHIRIKI KATIKA MAZISHI YA KAMANDA MWENZAO!!

0 comments:

Chapisha Maoni

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595