Kenya imewasilisha rasmi barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
kuahirisha kesi zinazoendelea katika mahakama ya ICC dhidi ya rais
Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto. Pia, nchi 49 za Umoja wa
Afrika zimetia saini barua iliyowasilishwa Jumanne kwa baraza hilo
ikiunga mkono kuahirishwa kwa kesi hizo dhidi ya viongozi wa Kenya.
balozi
wa Kenya katika Umoja wa Mataifa bw. Macharia Kamau alisema Kenya na
Umoja wa Afrika wanasubiri kwa hamu maamuzi ya Baraza hilo
Katika
ombi lake Kenya inalitaka Baraza hilo kufikia maamuzi ya haraka
kuwawezesha viongozi wake kutohudhuria vikao vya kesi dhidi yao katika
mahakama ya The Hague kwa mwaka mmoja.
Viongozi hao wa Kenya wanakabiliwa na mashtaka mbele ya mahakama ya
kimataifa ya ICC kwa tuhuma kwamba walichochea ghasia za baada ya
uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 na mapema mwaka wa 2008.
Kesi dhidi ya naibu rais Ruto imekuwa ikiendelea, huku kesi dhidi ya bw.
Kenyatta ikitazamiwa kuanza Novemba 12 mwaka huu. Aidha balozi Kamau
anasema anatazamia maamuzi ya Baraza hilo yatafikiwa kwa wakati ili
rais huyo aweze kupanga mikakati ya ulinzi wa taifa lake ambao ni
muhimu sawa na wa nchi nyingine yoyote duniani.
Balozi Kamau alisema Kenya inakabiliwa na tishio kuu la ugaidi na
ukosefu wa usalama hata kutoka pembe ya Afrika. Alisema ombi la Kenya
la mwaka wa 2011 katika Baraza hilo halikupata majibu yaliyotegemewa na
kwamba viongozi wake bw. Kenyatta na naibu rais Ruto wanahitaji kuwa
nchini kusimamia shughuli za usalama na majukumu yao kama wanavyotakiwa
na katiba ya nchi hiyo.
Alhamisi, 24 Oktoba 2013
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Call Us Now:
+255 655 732121,
+255 716 758595 / +255 762 758595
0 comments:
Chapisha Maoni