Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati akiwa
katika picha ya pamoja na Andrew Nyerere Mtoto wa Kwanza wa Baba wa
taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wakati alipozuru kaburi la Mwaasisi
huyo wa taifa la Tanzania Mwitongo, Butiama Nyumbani kwa mwalimu Mkoani
Mara jana, Kinana alifanyakazi na Andrew Nyerere
wakati wakilitumikia Jeshi la Ulinzi la wananchi la Tanzania (JWTZ),
Katibu Mkuu huyo jana aliendelea na ziara yake katika wilaya ya Butiama
katika kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya
Chama cha Mapinduzi, Kinana ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya
Serengeti leo. Kushoto ni Nape Nnayue Katibu wa (NEC) Itikadi Siasa na
Uenezi.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu
kutoka kulia akiongozwa na ndgu wa Mwalimu Mzee Jack Nyamwaga wakati
akielekea kuweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius K. Nyerere jana mjini Butiama, Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Butiama Mama Mabula
Mbunge
wa Jimbo la Musoma vijijini Mh. Nimrod Mkono akitoa maelezo mbele ya
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akikagua ujenzi wa
zahanati Busegwe
Katibu
Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa
mgolole na Katibu wa kabila la Zanaki Mzee Peter Nyamrubwe Nyamrubwe
kama ishara ya kuwa mmoja wa viongozi wa kimila wa kabila la wazanaki,
kulia ni Mh Nimrod Mkono Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini.
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuangalia Katibu Mkuu wa UWT Taifa Bi. Amina Makilagi wakati akishiriki kucheza ngoma.
Jumapili, 22 Septemba 2013
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Call Us Now:
+255 655 732121,
+255 716 758595 / +255 762 758595
0 comments:
Chapisha Maoni