Jumatatu, 20 Mei 2013

SHERIA YA KUSIMAMIA VYOMBO VYA HABARI KUWASILISHWA BUNGENI

IMG_1500                                   
Serikali imeridhia kutungwa kwa sheria ya Kusimamia vyombo vya Habari ambapo muswada wa kutunga sheria hiyo utawasilishwa bungeni hivi karibuni.

Akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara yake bungeni mjini Dodoma leo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara alisema baada ya sheria hiyo kupitishwa na bunge, Wizara itaanza kuandaa waraka wa mapendekezo ya kutunga sheria ya Haki ya kupata Habari wakati serikali ikiendelea na utafiti ili kupata uzoefu kutoka nchi mbalimbali zenye sheria hii.

Kwa mujibu wa Dkt. Mukangara kutungwa kwa sheria ya kusimamima vyombo vya habari kutasaidia katika kuimarisha tasnia ya habari nchini na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zinazoikabili wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo likiwemo suala la mafunzo kwa waandishi wa habari pamoja na mazingira duni ya kazi.

Katika hotuba yake Dkt. Mukangara alisema pia Wizara yake imeazimia kutekeleza suala la uanzishwaji wa benki ya Vijana ya Taifa katika mwaka wa fedha wa 2013/2014.

Aliongeza kuwa Wizara pia itaboresha huduma ya Mfuko wa Maendeleo ya mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana pamoja na kuendelea kuzijengea uwezo SACCOS zinazotoa huduma kwa vijana.

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inaomba kuidhinishiwa bajeti ya jumla ya shilingi 21,328,045,000 ambapo kati ya fedha hizo, fedha za matumizi ya kawaida ni 20,728,045,000 na fedha za miradi ya maendeleo ni shilingi 600,000,000

Call Us Now:

+255 655 732121, +255 716 758595 / +255 762 758595